Fundi Sanifu wa Mradi wa Maji Mbagala Rufu Robert Chenge
akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe baada ya
kutembelea mradi wa Mbagala Rufu uliofanyiwa maboresho na Mamlaka ya
Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe akizungumza na
wananchi wa Jet watakaopata huduma ya maji kupitia mradi wa Jet Buza
unaotarajiwa kumalizika mwezi Aprili mwaka huu, mradi wa maji wa Jet
Buza unasimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es
Salaam (DAWASA) unaohudumia takribani wakazi 10,000
Katika maeneo ya Kiwalani, Jet, Buza hadi Mwanagati.
Meneja wa Mkoa wa Kihuduma Dawasa Temeke
Crosman Makere akitolea ufafanuzi mradi wa maji aa Jet - Buza kwa Mkuu
wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe unaotarajiwa kumalizika mwezi Aprili
mwaka huu wenye thamani ya Bilion 3.7 mradi huo utahudumia wakazi wa
Kiwalani, Jet, Buza hadi Mwanagati.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe akimtwisha mama
ndoo ya maji baada ya kutembelea mradi wa Mbagala Rufu uliofanyiwa
maboresho na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam
(DAWASA.)
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe akizungumza na
wananchi wa Kata ya Mbagala alipotembelea mradi wa maji wa Moringe
unaosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es
Salaam (DAWASA) unaohudumia takribani wakazi 3,000 wa kata hiyo
Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv
MKUU wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe amesema Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kutumia lugha nyepesi ya
mawasiliano kutoa elimu kwa wananchi juu ya huduma zinazotolewa na
mamlaka hiyo.
Mkuu wa Wilaya amefanya ziara ya kutembelea miradi ya Dawasa ndani ya
Wilaya hiyo akianzia mradi wa maji wa Jet- Buza unaotarajiwa
kumamilika mwezi April mwaka huu na kisha kutembelea miradi ya Jamii
katika sehemu tatu tofauti.
Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya
amesema Dawasa wanatakiwa kutumia lugha nyepesi wakati wa kutoa elimu
juu ya bei ya huduma ya maji inayotolewa na Mamlaka hiyo.
Amesema, Dawasa wanafanya kazi kubwa sana ya kutoa huduma ya maji
ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam lakini wananchi wengi wanashindwa
kutumia huduma hiyo kwa kudhania bei ni kubwa lakini kuna tofauti
kubwa sana na gharama za watu binafsi na zile za Dawasa.
"Unajua ukinunua lita 20 ya maji unauziwa kwa sh 100 lakini ukipiga
mahesabu kwa huduma wanayotoa Dawasa ya Unit 1 kwa sh 1663 ni sawa na
kununua ndoo moja ya maji kwa sh 33.3 ambapo mwananchi unakuwa
umenusuru kiasi kikubwa cha fedha ikiwa ni kwa mwezi ah mwaka."
amesema Gondwe.
Aidha, ameupongeza uongozi wa Dawasa chini ya Afisa Mtendaji Mkuu
Mhandisi Cyprian Luhemeja amefanya kazi kubwa ya kuhaakikisha wananchi
wanapata huduma ya maji na miradi yote inafanya kazi kama hivi
mnavyoona.
"Nimpongeze Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa ameonyesha uweledi wa nafasi
aliyopewa, waananchi wa Temeke sasa hivi wanapata huduma ya maji safi
kuna maeneo yalikua na changamoto ya maji hasa kwenye miradi ya muda
mrefu kama hii lakini wao kama Mamlaka wamechukua na wameifanyia kazi
na mnafurahia huduma ya maji."
Akiwa katika mradi wa maji Mbagala Rufu uliotumia takribani milion 78,
Gondwe amewapa siku saba mamlaka hiyo kukamilisha ofisi na kuanza
kuongeza mtandao wa mabomba katika maeneo ambayo hayajapata mradi huo.
Kwa Upande wa Meneja wa Mkoa wa Kihuduma Temeke Crosman Makere
akizungumzia miradi aliyotembelea Mkuu wa Wilaya Temeke, amesema mradi
wa Jet Buza una thamani ya Bilion 3.7 na unatarajiwa kukamilika mwezi
Aprili mwaka huu ukilazwa mabomba ya inchi 16 kwa urefu wa Km 7.5 na
km 37 kwa mabomba ya usambazaji maji.
Amesema, kwa sasa mafundi wapo kazini wakiendelea na shughuli za
ulazaji wa mabomba hayo sambamba na kuanza maunganisho kwa wateja
wapya wa Dawasa walioomba huduma ya maji na utahudumia wakazi 10,000
(elfu kumi.)
"Kwa mradi wa Mbagala Rufu, Dawasa iliuchukua mradi huu ukiwa hauko
katika hali nzuri tumeufanyia ukarabati tukitumia Milion 78 na hata
mradi wa Moringe ni Milion 54 tukiongezea vizimba vya kuchotea maji,
kuongeza mtandao wa maji na ununuaji wa matanki ya kuhifadhia maji."
amesema Makere
Aidha, amesema kwa sasa jumla ya wateja zaidi ya 250 katika miradi
hiyo ya kijamii na wananchi wanaendelea kuomba kuunganishwa kupata
huduma ya maji.
Ziara ya Mkuu wa Wilaya ilihitimishwa kwa kuwataka wananchi kulinda
miundo mbinu ya maji kwani fedha zinazotumika ni za serikali ambapo
utakapoharibu miundo mbinu hiyo wananchi wengine watakosa huduma ya
maji na kuwataka kutoa taarifa pindi wanapoona mtu amefanya uharibifu
wa miundo mbinu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...