NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezitaka idara za ardhi katika halmashauri za mkoa wa Shinyanga kuwatambua wamiliki wote wa ardhi ambao ramani za upimaji wa viwanja vyao umeidhinishwa na kuanza kuwatoza kodi ya pango la ardhi kwa mujibu wa sheria.
Dkt. Mabula alitoa agizo hilo tarehe 01 Februari 2021 mkoani Shinyanga wakati wa ziara yake ya siku moja kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi, kuhamasisha ukusanyaji kodi ya pango la ardhi pamoja na kukutana na makampuni ya urasimishani.
" kila halmashauri katika mkoa huu wa Shinyanga ichukue hatua kwa kuwatambua wamiliki wote wa viwanja ambao approved survey imefanyika na kuanza kuwatoza kodi ya pango la ardhi." Alisema Dkt Mabula.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...