Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
MAKAMU
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze ,Bagamoyo Mkoa wa Pwani Ismail
Msumi, ametoa wiki mbili kwa viongozi wa Kijiji cha Kimange kumaliza
deni la maji, ili wananchi waendelee kupata huduma.
Msumi
ametoa kauli hiyo katika mkutano kwenye Kitongoji cha Togo, baada ya
mkazi aliyejitambulisha kwa jina la Said Mohamed kuelezea changamoto ya
huduma hiyo.
Alisema kwa muda mrefu wanalazimika kutumia maji ya tenki la shule ya sekondari Kimange.
"Katika
eneo letu maji yamekatwa kutokana na deni linaloelezwa limesababishwa
na aliyekuwa ana simamia kituo cha kuchotea maji, kabla ya kufungwa kwa
bomba hilo, ukienda kwenye mabomba mengine kipindi cha mvua maji
yanapatikana, kiangazi hayapatikani," alisema mkazi huyo.
Wakitolea
ufafanuzi kuhusiana na kilio hicho, Mwenyekiti wa Kijiji Said Bakar na
Mtendaji wake Mariamu Selemani walisema kuwa sababu zinazosababisha
kukosekana kwa maji kunatokana na deni, ambapo walikwenda kwenye ofisi
za DAWASA Chalinze wakaambiwa wanatakiwa kulipa
"Juhudi
mbalimbali tumezichukua ikiwemo aliyekabidhiwa kituo cha kuuzia maji,
ambapo alisema changamoto hiyo imetokana na yeye kukumbwa na matatizo ya
kifamilia huku akiahidi kulipa deni hilo," alisema Mwenyekiti huyo.
Ofisa
Mtendaji wa Kijiji hicho alisema kwamba baada ya kupewa agizo la kulipa
fedha hizo hajapewa mrejesho kama ameshalipa au la, huku akiahidi
kulifanyiakazi suala hilo ili huduma ya maji iendelee kupatikana kwa
wananchi.
Baada ya
maelezo hayo Msumi akasema anatoa wiki mbili mdaiwa huyo awe amelipa
deni hilo, kinyume chake atawawajibisha viongozi wote we Kitongoji na
Kijiji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...