Charles James, Michuzi TV

MBUNGE wa Mtama, Nape Nnauye (CCM) ameishauri serikali kupitia  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),kuacha kutumia 'Task force' ambayo inaua  na kutumia wataalamu katika ukusanyaji kodi.

Nape  ameyasema hayo leo bungeni alipokuwa akichangia Mapendekezo ya mwongozo wa maandalizi ya mpango, bajeti ya serikali na mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka 2021/22.

Nape amesema  "Ukusanyaji wa kodi ni taaluma lakini changamoto ni kwamba tumeamua kutumia task force kukusanya kodi, kwasababu sio taaluma yao wanakwenda kuua biashara, wanakwenda kwa mfanyabiashara hawajali maisha yake ya kesho, tunafurahia matokeo ya kukusanya kodi lakini biashara zinazofungwa ni nyungi, kesho hatuna wa kumkamua maziwa,”

Amefafanua kuwa  kelele zinazosikika ni kwa sababu wameacha kutumia taaluma ya ukusanyaji kodi kwa sababu sio taaluma yao wanachoangalia ni kufikia lengo.

“Kuna sehemu wanakwenda tayari na kesi za uhujumu uchumi, wanawatisha watu, watu inabidi watoe fedha na wanafunga biashara zao…Sasa kinachotokea wakienda kwa mfanyabiashara hawajali maisha yake ya kesho,sasa tunafurahia matokeo ya muda mfupi lakini haya matokeo ni ya muda mfupi kwa sababu idadi ya biashara zinazofungwa ni nyingi mno,” Amesema Nape.

Hata hivyo, Mbunge huyo ametoa ushauri kwa Serikali kupunguza kukusanya kodi kwa njia ya task force na badala yake watumie wataalamu.

MBUNGE wa Mtama,Mhe. Nape Nnauye (CCM)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...