MkuuwaMkoa wa Singida Dtk. RehemaNchimbi katikati akiongoza Kongamano la Fursa za Uwekezaj ikwenye Mkoa wa Singida, Kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Lucy Sheen, kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi.
Wakuu waWilaya zaMkoawaSingida(kwenye mstari wa kwanza) wakifuatilia Mada mbalimbali wakati wa Kongamano la uwekezaji Mkoani Singida. AfisaUhamasishaji Uwekezaji Mkuu kutoka Kituo cha Uwekezaji nchini, Joyce Shundu akiwasilisha mada ya“Mazingira na Fursa za Uwekezaji Nchini”amepongeza jitihada na mikakati mbalimbali inayofanywa na MkoawaSingida 

Viongozi wa Wachimbaji Madini Mkoa wa Singida wakiwa kwenye banda lao wakionyesha madini mbalimbali kwa wadau waliotembelea banda la wachimbaji wa madini Mkoa wa Singida (SIREMA).


Wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo wakionyesha bidhaa zao


RAS ASEMA MKOA UMEJIANDAA KIKAMILIFU

Na John Mapepele, Singida

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe, Dkt. Rehema Nchimbi amewataka Wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja kuwekeza kwenye Mkoa wa Singida kwa kuwa Mkoa huo umebarikiwa kuwa na fursa mbalimbali za uwekezaji ambazo bado hazijatumika kikamilifu.

Akifungua Kongamano la Mwongozo wa Uwekezaji kwenye Mkoa wa Singida kabla ya uzinduzi rasmi wa mwongozo huo, Dkt. Nchimbi amesema Mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa michache nchini ambayo endapo fursa zake zikitumika utachangia katika maendeleo ya Mkoa na nchi kwa ujumla

Amezitaja baadhi ya fursa zilizopo kwenye Mkoa wa Singida kuwa ni pamoja na nishati ya mafuta asilia na gesi, madini, kilimo cha alizeti, korosho,utalii, ufugaji wa nyuki na kuku pia uwekezaji kwenye sekta ya michezo ambapo amesema ni zamu ya Mkoa wa Singida kuchangia kikamilifu kwenye uchumi wa nchi.

Akitoa mada kuhusu Uwekezaji wa Alizeti mkoani Singida, Mratibu wa Utafiti wa Alizeti nchini, Frank Reuben amesema zao la alizeti ndiyo zao pekee linaloweza kuuvusha mkoa wa Singida kwa kuwa tafiti zinaonyesha kuwa mkoa wa Singida ndiyo unaongoza hapa nchini kwa kulima zao hilo.

Ametaja baadhi ya maeneo ya fursa za uwekezaji kwenye kilimo cha Alizeti kuwa ni pamoja na uzalishaji na usambazaji wa mbegu, Kilimo bora (mesto) cha alizeti na ufugaji nyuki (Agro-apiculture) na uendelezaji wa viwanda vya kuchakata alizeti, chakula cha mifugo na mazao ya nyuki

Mtafiti wa zao la Korosho, kutoka Taasisi ya Utafiti wa mazao ya Kilimo (TARI) Dkt. Fortunatus Kapinga akitoa mada ya zao la Korosho nchini amesema Mkoa wa Singida una ardhi nzuri yenye rutuba ambayo inafaa sana kwa zao la korosho ukilinganisha na mikoa mingine hapa nchini hivyo ni fursa pekee kwa wawekezaji kuja kufanya uwekezaji katika mkoa huu.

Amezitaja baadhi ya bidhaa zinazopatikana kwenye zao la Korosho kuwa ni pamoja na juisi, jamu,mvinyo, maziwa na siagi ambapo amesema kauli mbiu ya mkoa kwenye uwekezaji kwamba “ni zamu yetu” ikitafsiriwa kwa vitendo italeta mageuzi makubwa katika mkoa wa Singida na taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti wanawake wachimbaji Madini Mkoa wa Singida, Martha Kayaga amepongeza Serikali ya awamu ya Tano inayoongizwa na Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kwa jitihada kubwa inayofanya kuwashilikisha wachimbaji wazawa kwenye sekta ambapo ameiomba Serikali kuangalia namna bora ambayo itawawezesha wajimbaji wadogo wadogo kupata mitaji hususan vifaa ili waweze kuongeza tija katika sekta hiyo.

Pia Bi. Kayaga ameiomba Serikali kuwaangalia wachimbaji wanawake kwa jicho la pekee kwa kuwa wao ni nguzo muhimu kwenye familia na kwamba asilimia 10 inayotengwa kwenye Halmashauri imekuwa ikielekezwa kwenye sekta nyingine ambapo amesisitiza endapo itaelekezwa kwa akina mama wachimbaji wadogowadogo itasaidia kuinua hali za uchumi kuanzia kwenye ngazi ya kaya na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake, Afisa Uhamasishaji Uwekezaji Mkuu kutoka Kituo cha Uwekezaji nchini, Joyce Shundu akiwasilisha mada ya “Mazingira na Fursa za Uwekezaji Nchini” amepongeza jitihada na mikakati mbalimbali inayofanywa na Mkoa wa Singida kwa kwenye uwekezaji na kutoa wito kwa wawekezaji kuwahi kuwekeza kwenye fursa za kipekee zinazopatikana mkoani hapa.

Awali katika salamu za utambulisho, Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi amewataka Watendaji wote wa Serikali Mkoa wa Singida kuhakikisha wanajituma kufanya kazi kwa weledi kwenye utoaji huduma bora kwa wawekezaji ili azma ya Serikali ya kutaka uwekezaji wenye tija itimie na maisha bora kwa watanzania ifikiwe.

Dkt. Lutambi amesema Serikali ya Mkoa imeshaandaa mazingira wezeshi kwa wadau na wawekezaji makini kuja kuwekeza kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...