Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akionesha Tuzo aliyokabidhiwa na Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kinondoni kwa kutambua mchango wake mkubwa alioutoa kwa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam, wakati wa Maadhimisho ya kutimia miaka 44 ya Chama cha Mapinduzi CCM yaliyofanyika leo Febuari 06,2021 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwabwepande Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiweka jiwe la msingi Ujenzi wa Jengo la Hospitali ya Kisasa ya Wilaya ya Kinondoni katika eneo la Mwabwepande Jijini Dar es salaam leo Febuari 06,2021. kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Mama Kate Kamba.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Tuzo kutoka kwaMwenyekiti wa CCM Wilaya yua Kinondoni Cde, Harold Maruma kwa niaba ya  Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kinondoni kwa kutambua mchango wake mkubwa alioutoa kwa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam, kwenye Maadhimisho ya kutimia miaka 44 ya Chama cha Mapinduzi CCM yaliyofanyika leo Febuari 06,2021 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwabwepande Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...