***************************************
Na Mwandishi wetu, Simanjiro
WAZIRI Mkuu mstaafu Mizengo Peter Kayanza Peter Pinda na mlezi wa CCM Mkoa wa Manyara, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, jana katika muendelezo wa matukio mbalimbali ya kuadhimisha sherehe za miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM, akiwa Wilayani Simanjiro.
Mh. Pinda pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali ametembelea mradi wa maji kata ya Terrat, Kijiji cha Longsone,
Mradi wa maji kata ya Loiborsiret Kijiji Cha Narakauo
Na mradi mkubwa kabisa wasmaji kutoka mto Ruvu kwenda makao makuu ya wilaya ya Simanjiro (Orkesumet)
Katika miradi yote aliyotembelea mlezi amejionea jitihada za serikali ya awamu ya tano kupitia Ruwasa.
Pia Mh. Pinda amesisitiza miradi hiyo kukamilika kwa wakati na kutunzwa vizuri ili kuwasaidia wananchi was maeneo husika kunufaika na huduma hiyo ya maji kwa wakati na kwa muda mrefu zaidi.
Tunakushukuru Sana mlezi wetu kwa kazi nzuri uliyoifanya na unayoendelea kuifanya katika mkoa wetu. Tunakuombea nguvu na afya njema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...