HATIMAYE aliyekuwa Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Juma Abeid aliyekuwa kiongozi katika kipindi kilichopita amehukumuwa kwenda Jela kwa makosa ya kupokea rushwa kitu ambacho ni kinyume kabisa na sheria na taratibu za nchi zilizowekwa .
Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani imeeleza kuwa mnamo mwezi Novemba mwaka 2019 ilifungua mashitaka ya kuomba na kupokea rushwa dhidi ya mshitakiwa huyo Juma Abeid ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Mkuranga kabla ya kufanyika kwa uchaguzi Mkuu wa Viongozi wa mwaka 2020.
Kesi hiyo ambayo iliendeshwa katika mahakama ya hakimu mkazi Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani mbele ya hakimu mkazi Erieth Mwailolo .
Awali ilidaiwa kwamba Mshitakiwa alitenda kosa la kupokea hongo ili kumsaidia mwananchi (jina limehifadhiwa) ambaye alikuwa anahitaji uhamisho wa mke wake anayefanya kazi ya Ualimu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara kwenda Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Pia ilidaiwa mshitakiwa aliomba na kupokea kiasi cha Shilingi Laki mbili na elfu ishirini (Sh. 220,000/=) ili kuwezesha kufanyika kwa uhamisho huo kwenda Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga ambayo yeye alikuwa anaiongoza kwa nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo. Kitendo hiki ni kosa chini ya kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na 11 ya Mwaka 2007.
Hukumu ya kesi hiyo ilisomwa na hakimu mkazi Mheshimiwa Erieth Mwailolo mnamo tarehe 08 Februari, 2021 ambapo Mwenyekiti huyo wa Zamani Juma Abeid alihukumiwa kwenda jela miaka minne (4) au kulipa faini ya Shilingi laki saba (Sh.700,000/=) kwa kila kosa.
Mshitakiwa alikubali kulipa faini ya shilingi Milioni Moja na laki Nne (Sh. 1,400,000/=) na kuachiwa huru.
Picha ya mwonekano wa jengo la Mahakama ya hakimu mkazi Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...