JANUARI 28, 2021 Taasisi ya utafiti ya Kimataifa ya Transparency Internatuonal (TI,) imetoa taarifa ya hali ya rushwa duniani kwa kwa mwaka 2020 ambapo Tanzania imeshika nafasi ya 94 kwa kupata alama  38 kati ya nchi 180 huku ikielezwa kuwa matokeo hayo  ni kulingana na kiashiria cha 'CIRRUPTION PERCPTION IBDEX  (CPI,)  kilichoanzishwa  mwaka 1995 kwa lengo la kupima Hali ya RUSHWA katika nchi mbalimbali  duniani.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU brigrdia Jenerali John Mbungo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ambapo amesema kuwa;

''Itakumbukwa kwamba mwaka 2015 wakati Serikali ya  awamu  ya tano inaingia madarakani, takwimu za Transparency International za kupima hali ya rushwa Nchini zilionesha Tanzania imepata ALAMA 30/100 na kushika nafasi ya 117 kati ya nchi 180 zilizofanyiwa utafiti." Amesema Mbungo.

Brigedia Jenerali Mbungo amesema kuwa mafanikio hayo ni  makubwa kwani  Tanzania imepata alama 8 na kuzipita nchi 23 ndani ya miaka mitano tu. Kulingana na taarifa hiyo Tanzania imeshika nafasi ya pili katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, ikitanguliwa na Rwanda iliyopata alama 54.

Aidha katika taarifa hiyo inaonyesha kuwa Nchi ya Denmark na New Zealand zilishika nafasi ya kwanza duniani kwa kupata alama 88 huku Somalia na Sudani kusini zikishika nafasi ya 180 kwa kupata alama 12, kila mmoja.

"Ningependa Umma wa Watanzania ufahamu kwamba pamoja na mafanikio haya niliyoyataja, tatizo la rushwa nchini bado lipo. hivyo kuikabili kunahitaji wananchi pamoja na wadau wote kuendelea kushirikiana na TAKUKURU ili kuhakikisha kuwa vitendo vya Rushwa vinatolewa taarifa kwa TAKUKURU ili hatua stahiki za kisheria zichukuliwe.''  Amesema  Brigedia Jenerali Mbungo.

Hata hivyo Brigedia Jenerali Mbungo alimaliza taarifa hiyo kwa kusema;
 "Vita dhidi ya rushwa  ni ya wananchi wote kwa sababu huathiri watu wote. TAKUKURU ni jeshi dogo lililotangulia kwa wananchi wote.'' Amesema.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kwanini tunaamini hiyo ripoti iliyoandikwa na wazungu? Haiwezekani kuwa wanatudanganya sawa na chanjo ya Corona?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...