Na Woinde Shizza,  Michuzi Tv-Arusha

MKUU wa wilaya ya Karatu,  Abbas Kayanda amesema kuwa ni lazima
halmashauri ya Karatu  ikusanye mapato vizuri ili iweze kutekeleza
shughuli zake za miradi maendeleo,  na kueleza kuwa,  jukumu la madiwani ni kusimamia ukusanyaji wa mapato katika kata zao ili kuweza kufikia malengo ya waliojiwekea ya kukusanya kiasi cha billion nne na million mia tano
kwa mwaka huu wa fedha

Abbas Kayanda alisema hayo wakati akihutubia katika kikao cha kwanza
cha  baraza la madiwani ambapo alisema vyanzo vya mapato vilivyoainishwa kwenye bajeti visimamiwe vizuri, ili vitoe mapato yaliyokusudiwa.

Alisema wanahitaji madawa, wanahitaji kujenga zahanati, wanahitaji
kujenga madarasa wanahitaji kujenga nyumba za walimu, wanahitaji
kujenga lami Karatu na  vyote hivyo vinategemea namna watakavyokusanya
mapato.


Kayanda alisema kuna umuhimu wa wananchi kudai risiti za  za EFD pindi
wanaponunua bidha madukani ili kuongezea ukusanyaji mapato serikalini
na kuaendelee kufikiria  vyanzo vingine vya mapato ambavyo havijaguswa
katika maeneo   lazima washirikiane ili waweze kufikia malengo
waliojiwekea.

Akizungumzia kuhusu elimu  Kayanda alisema kuna fedha nyingi
zinazokusanywa kwa miradi mbalimbali ya elimu, hivyo wazo la kuunda
mfuko wa elimu litamsaidia kumpunguzia mwanachi, mzigo wa kuchangia
mara kwa mara ujenzi wa miundo mbinu ya elimu.

Alibainisha kuna kazi kubwa ya kufanya kuinua kiwango cha ufaulu kwa
elimu ya msingi, wakiimarisha mfuko wa elimu itatusaidia kuwapa
motisha walimu wanaofanya vizuri, katika shule za sekondari bado ufaulu hauko vizuri, na kuwataka kuwa na umoja wa namna ya kuondoa ufaulu wa daraja sifuri na daraja la nne,

 Kayanda alisema katika sekta ya afya kumekuwa na mwitikio wa chini
kwa wananchi kujiunga na mifuko ya bima ya afya ya jamii, hivyo
watawaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kujiunga katika mfuko wa
afya ya jamii iliyoboreshwa   wananchi wakijitokeza kujiunga na bima
ya afya vituo vyetu vya afya na zahanati vitaongeza upatikanaji  wa
madawa na vifaa tiba.

Aidha alisema bado kuna changamoto ya wakinamama kwenda kujifungua
katika vituo vya kutoa huduma za afya, lazima wakinamama wahamasishwe
kwenda kujifungua katika vituo vya huduma za afya,Vituo vya afya
visivyo katika mfumo wa ukusanyaji wa mapato kieletronic vinatakiwa
viwe na mfumo wa ukusanyaji wa mapato ili kuondoa upotevu wa
ukusaanyaji wa mapato.

Akizungumzia kuhusu ustawi wa jamii Kayanda alisema, halimashauri ya
Karatu ilitambua wazee 7776 kati ya wazee hao waliobahatika kupata
vitambulisho vya matibabu bure ni 3037, alibainisha kuwa ni  lazima
tujipime katika kipindi cha miaka mitano, tutaifanyia nini jamii yetu.

Naye  Mwenyekiti wa Halmashauri  John Lucian Mahu alisema baada ya
baraza kujigeuza kamati imepitisha wazo la kuanzisha mfuko wa elimu wa
wilaya ya Karatu,  wazo limekuja kwa sababu wamekuwa wakisuasua sana
katika kuinua kiwango cha ufaulu, wazo hilo limeafikiwa lipelekwe
kwenye  kamati maalumu itakayoundwa na Mkurugenzi ambayo itasaidia
kuchakata na kupeleka maoni katika kamati tendaji ya Halmashauri (CMT)
ili ije na mapendekezo ya namna ya kutekeleza wazo la mfuko wa elimu
wa jimbo.

 Alisema baaada ya kujadiliwa mawazo hayo yatapelekwa katika kamati ya
 fedha na baada ya hapo itapelekwa kwenye baraza na tutaanzisha mfuko
wa elimu wa wilaya ya Karatu,wazo jingine lilojadiliwa na baraza
lilojigeuza kama kamati imeridhia kuhamisha mnada wa Karatu kwenda nje
ya mji wa Karatu ,ambapo kwa upande wa juu wa eneo la mnaada itajengwa
stand ya kisasa ya mabasi makubwa  na eneo la upande wa chini
utajengwa uwanja wa mpira wa kisasa na viwanja vingine vya michezo na
upande mwingine wa eneo hilo watajenga ukumbi wa kisasa wa mikutano wa
Halmashauri.

 Aidha alisema kuwa  kamati pia imeridhia kujengwa kwa hosteli za
wasichana na hosteli za wavulana kama sehemu mojawapo ya kubuni vyanzo
vipya vya mapato katika eneo hilo la uwanja wa mnadani, zoezi la
kuhamisha eneo la mnada litafanyika taratibu na mnada utapelekwa
katika eneo jingine nje ya mji, Stenndi ya sasa ya mabasi itatafutiwa
kazi nyingine kadri itakavyoonekana inafaa

Mahu alisema lazima tushirikiane kwa pamoja wataalamu na watendaji ili
tuwafute machozi wananchi,  kusimamia mapato sio kazi ya mkurugenzi ni
kazi ya wote ili tuweze kupunguza madeni wanayodaiwa kama Halmashauri

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri  Waziri Mourice
alisema utaratibu mzuri utawekwa kwa ajili ya kuunda mfuko wa elimu wa
jimbo,mfuko wajimbo hautagusa wazee wenye umri wa miaka 60 na
kuendelea ,mfuko utakusanya michango kwa wananchi wenye umri wa miaka
18 -59,pia elimu imeboreshwa na hivyo wanatarajia ongezeko kubwa la
wanafunzi.

Akizungumzia kuhusu afya alisema kila kata inatakiwa iwe na kituo cha
afya na kila kijiji kinatakiwa kiwe na zahanati lakini hawana zahanati
kila kijiji ambapo wana kata 14 ambazo kila kata inatakiwa kuwa na
kituo cha afya lakini kwa sasa serikali inavituo 5 vya afya, hali hiyo
inasababisha vituo vya afya kuzidiwa kutokana na wingi wa watu
kutokana na ubora wa huduma na bei nafuu zinazotolewa katika vituo vya
afya vya serikali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...