Katibu wa umoja wa wavunaji miti mkoa wa Iringa (UWASA)Dr Bazir Tweve akipokea miche ya miti kwa niaba ya wananchi wengine mbele ya Mhifadhi Mkuu wa Shamba la miti la Sao hill Juma Mwita
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Wadau wa misitu mkoani Iringa
wameipongeza wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti
la Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindi kwa kugawa miti milioni moja kila mwaka
kwa wananchi na taasisi mbalimbali zinazolizunguka shamba hilo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa miche ya miti ,katibu wa umoja wa wavunaji miti mkoa wa Iringa (UWASA)Dr Bazir Tweve alisema kuwa uongozi wa shamba la Sao Hill umekuwa ukitoa miti na elimu ya utunzaji wa miti kwa wananchi wanalizunguka shamba hilo.
Alisema kuwa wamekuwa wakitoa
elimu ya uhifadhi misitu kwa wananchi na wadau mbalimbali wanajihusisha
nawasiojihusisha na zao la miti kwa kuendelea kutunza na kulinda mazingira
yasihalibike kwa njia mbalimbali kama vile kuchoma moto au kukata miti hovyo.
Dr Tweve aliongeza kuwa kitendo
cha TFS Mufindi kutoa miche milioni moja kunasaidia kuwakumbusha wananchi
kupanda miti na kuitunza vizuri hadi pale itakapofika muda wa kuvunwa kutoakana
na aina ya mitia ambayo wameipanda.
Dr tweve aliwaomba uongozi wa wakala
wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti la Sao Hill lililopo
wilaya ya Mufindikutoa elimu ya uvunaji wa miti ili kuepukana na wananchi
kuvuna miti ikiwa bado haijakomaa kuvunwa na kupeleka bidhaa ambayo haihitajiki
sokoni.
Naye Mhifadhi Mkuu wa Shamba la
miti la Sao hill Juma Mwita alisema kuwa wameyapokea mawazo ya wadau na kuahidi
kuyafanyia kazi ikiwapo swala la kutoa elimu kwa wananchi wanaovuna miti mapema
kabla ya muda wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...