Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini Tanzania Wilbroad Mutafungwa akizungumza na Madereva pamoja na mawakala wa mabasi katika Standi kuu ya Mabasi Mkoani Arusha.
Kamanda wa kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini Tanzania Wilbroad Mutafungwa akiwa pamoja na mkuu wa Usalama barabarani mkoa wa Arusha,DTO,Katibu wa RSA mkoa wa Arusha Willard Ngambeki,pamoja na Mabalozi wa Usalama barabarani RSA waliovaa t-shirt.
Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Solomoni Mwangamilo akimsikiliza mmoja wa dereva katika Stendi ya Dar Express Mkoani Arusha.

Na.Vero Ignatus,Arusha
Wito
umetolewa kwa wamiliki wa mabasi ya safiri safari ndefu ,kuhakikisha kwamba
yanakuwa na madereva wawili ,lengo likiwa ni kupunguza ajali zinazoweza
kuepukika, pale dereva anapochoka kutokana na kuendesha gari kwa umbali mrefu
Hayo
yamesemwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani nchini Wilbroad
Mutafungwa ,alipokuwa kikazi mkoani Arusha mwishoni wa juma kwamba, ameshatoa maelekezo kwa akwuu
wa usalama barabarani kwa mikoa yote ,kuhakikisha wanafanya ufuatiliaji wa kina ,sambamba na
suala zima la mashindano ya mabasi ya abiria barabarani
Amewataka
madereva wote nchini kuacha mashindano barabarani ,ambayo hayana maana yeyote
kwani mara nyingi wamekuwa wakisababisha ajali vifo ,majeruhi na ulemavu wa
kudumu pamoja na kuleta hasara,jambo ambalo wangelifuata utaratibu na
kuzingatia sheria za usalama barabarani yote hayo yasingelitokea.
‘’Wapo baadhi
ya maajenti ambao sasa ndiyo vichocheo vikubwa, nikiwa na maana kwamba wanafanya ile michezo ya kubeti ,gari linalofika sehemu Fulani
ikiwa ya kwanza wanabeti wanachangishana fedha.Alisema Mutafungwa.
Kamanda Mutafungwa amewaagiza
wakuu wote wa usalama barabarani, wawakamate maajenti ambao ndoyo wanaochochea
kubeti,kushangilia ,kuwachochea madereva ili waweze kukimbia mwendokasi, pamoja
na dereva mwenyewe kwani ‘’Hatuwezi kubeti na Maisha ya watu’’
Vilevile Kamanda
Mutafungwa alipata wasaa wa kuzungumza na abiria waliokuwa katika stendi ya mabasi
Arusha :Ninyi ndiyo wadau muhimu katika suala la usafiri, hivyo mnalojukumu
kubwa sana la kutusaidia,kuna mahala penine askari wetu wa usalama barabarani
hawapo,mnapoona kuna uendeshaji wagari unaovunja sheria za usalama barabarani
kwa makusudi na wakati mwingine katika kiwango ambacho kinaweza kuhararisha hata
maisha yenu, nawaombeni ndugu zangu abiria ,toeni taarifa kwa jeshi la polisi ili
tuweze kumchukulia hatua za kisheria.
Wapo abiria tunapotembea tunawaona wanashabikia sana spidi niwaombe kwasababu leo wewe ni abiria kesho siyo abiria kama Watanzania tujenge tabia ya kuona maovu na kuyakemea kwa pamoja .alisema
Mutafungwa amesema kuwa wapo baadhi ya madereva ambao hawajaacha tabia ambayo imepigwa marufuku ya uendeshaji wa magari kwa mwendo kasi huku wakiwa wamebeba abiria,Unakuta baadhi ya madereva sehemu ambayo anatakiwa kwenda spidi 80,bado anakwenda spidi kubwa zaidi ya hiyo,sehemu abayo ni makazi ya watu anapotakiwa kwenda spidi ya 50, bado baadhi ya madereva wanakwenda mwendo kasi n hata sehemu ya zebra crossing tunashuhudia hayohayo yakitendeka
Herman Malisa ni dereva wa marangu coach alikuwa na haya ya kusema: Ninachowaomba Madereva wenzangu tuzingatie kanuni na sheria za Usalama barabarani,kwani hiyo ndiyo ofisi yetu na wanatakiwa kuiheshimu kwa kutii Sheria bila shuruti
Amewataka kuwa makini sambamba na kuwajali abiria wao kwani wao ndiyo sababu ya wao kuwepo katika vyombo hivyo,sambamba na kuwataka kutokulaghaiwa na maajenti ambao hawana nia njema ,ambao wanawashawishi baadhi ya madereva kukimbiza magari na kutokuzingatia sheria za usalama barabarani
kwa upande wake Katibu wa mabalozi wa usalama barabarani mkoa wa Arusha Wilbald Ngambeki amesema kuwa wao kama RSA Kutoa elimu kwao ni ibada ,kwani elimu hiyo inawasaidia watu wengi ikiwemo abiria kutambua haki yake ya msingi awapo safarini ambayo inampa yeye nafasi ya kutoa taarifa pale anapoona dereva anakiuka sheria za usalama barabarani.
Ngambeki aliwataka abiria kutokuwa chanzo cha vichocheo vya kumshawishi dereva kutembea kwa mwendo kasi ,kwani tatizo litakapotokea majuto anakuwa mjukuu baadae na madhara yanakuwa makubwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...