NA  YEREMIAS  NGERANGERA….NAMTUMBO

Dereva  wa pikipiki   katika kijiji cha Mgombasi   wilayani Namtumbo  mkoani  Ruvuma  Kaimu  Kinokwite (28) amekufa kwa kukatwa  shingo  na waya  wa umeme baada ya kunaswa  na waya uliokuwa  umekatisha  barabara .

Kwa  mujibu  wa  walioshuhudia tukio hilo akiwemo mwalimu mkuu  wa shule ya msingi  Mgombasi Hance  Mwailima alisema  kuwa walimwona  kijana huyo akirushwa kutoka katika pikipiki na kutupwa mbali baada ya kunaswa na waya huo.

Mwailima  alidai marehemu alimbeba abiria wakitokea  mgombasi madukani (kijiweni) wakielekea  kijiji cha Mtumbatimaji  katika harakati za kununua mahindi na walipofika katika kitongoji cha Dodoma jirani na shule ya msingi Mgombasi walipatwa na mkasa huo na mwenzake alikimbia .

Aidha mwailima alidai katika eneo hilo la tukio hapakuwa na alama yoyote iliyowekwa  kuashiria kuwa kuna kazi ya kuweka nyaya  za umeme  katika nguzo za umeme  hali iliyomfanya dereva wa bodaboda huyo  kukumbana na mkasa akiwa katika mwendo kasi .

 Kaimu mtendaji wa kijiji cha Mgombasi  bwana Saidina Assedi  Sandali alikiri kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa marehemu alifikishwa kituo cha afya Namtumbo licha ya kuwa alishafariki  katika eneo la tukio .

Mtendaji wa  kata ya Mgombasi  bwana David  Julius  Kitalika pamoja na kukiri kutokea kwa  kifo hicho aliwataka  madereva wa pikipiki  kuwa waangalifu muda wote wakiwa barabarani hasa katika kipindi hiki cha utengenezaji   na uwekaji nyaya  za umeme  unaendelea katika vijiji vya kata ya mgombasi.

Marehemu  karimu  alizikwa katika makaburi ya minazini kata ya Rwinga  katika mamlaka ya mji mdogo wa Namtumbo  wanakoishi wazazi  wake.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...