Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wamekumbushwa kuacha uoga na kufanya kazi kwa weledi, maarifa na kulingana na nafasi walizokuwa nazo.
Hayo
yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja
katika kikao kilichofanyika na Madereva wa Mamlaka mwishoni mwa wiki.
Akizungumza
wakati wa kikao hicho, Afisa Mtendaji Mkuu Mhandisi Cyprian Luhemeja
amesema kada ya udereva ni kada muhimu katika utumishi wa umma hivyo
lazima waheshimu kazi yao.
Amesema
mkutano huo na madereva unalenga kuzungumza nao masuala mbalimbali ya
kimkakati katika kuboresha ufanisi upande wa nafasi za udereva kwani nao
ni kada muhimu katika watumishi wa umma na ndiyo watendaji wakuu wa
kazi za kila siku.
Mhandisi
Luhemeja amewakumbusha watumishi hao kutunza vitendea kazi vyao ambavyo
ni Magari huku akiagizia idara ya masuala ya usafiri kutokubadilisha
madereva bila idhini yake.
"Nataka
watumishi ninyi kutunza vitendea kazi vya Mamlaka sababu nyie ndio
mnayamiliki kwahiyo yawekwe katika hali ya usafi na natoa maagizo hakuna
madereva kubadilishwa bila idhini yangu," amesema.
Vile vile , Mhandisi Luhemeja amewakumbusha kufanya ukarabati (service) kwa wakati ili kutochelewesha shughuli za Mamlaka.
Afisa
Mtendaji Mkuu amekuwa na utaratibu wa kukutana na watumishi wa kada
tofauti tofauti na kujadili nao masuala mbalimbali na kutatua changamoto
ili malengo ya taasisi yaweze kufikiwa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa
Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza
na madereva wa Taasisi hiyo wakati wa kikao chake na kuwataka waache
uoga na kufanya kazi kwa uweledi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...