Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), leo imeungana na viongozi pamoja na wananchi wa wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma katika zoezi la upandaji miti ikiwa ni sehemu ya mpango wa kampuni hiyo wa kutunza mazingira.

 Spika wa Bunge Job Ndugai na viongozi wa Halamashauri ya Wilaya ya Kongwa walikuwa ni badhi ya viongozi walioshiriki katika zoezi hilo la upandaji miti lililofadhiliwa na SBL.

 Akiongea wakati wa zoezi hilo, mkurugenzi mtendaji wa SBL Mark Ocitti alisema upandaji miti katika wilaya ya Kongwa ni sehemu ya mkakati endelevu wa kampuni hiyo unaolenga kupanda maelfu ya miti sehemu mbali mbali hapa nchini.

 Mkurugenzi huyo alisema mwaka 2019 kampuni ya SBL ilipanda miti katika wilaya za Same Pamoja na Moshi ili kuongeza uotokatika maeneo ya jirani na mlima Kilimanjaro.

 “SBL inachukulia miti kama sehemu muhimu sana ya mazingira. Miti inasaidia kuhifadhi vyanzo vya maji, ni makazi kwa wanyama na wadudu mbali mbali, inavuta hewa chafu ya kaboni na kuzalisha hewa safi na pia miti ni chanzo cha dawa. Biashara yetu na jamii kwa ujumla ni sehemu ya mazingira na hii itunafanya kuwa jukumu letu sote kuyalinda na kuyatunza mazingira,” alisema Mark

 Upandaji miti wa SBL unakuja katika kipndi ambacho dunia inahangaika kupunguza uzalishaji ya hewa ukaa ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kuyalinda mazingira kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo

 Kwa upande wake Spika Ndugai aliishukuru kampuni ya SBL kwa kuunga mkono jitihada za upandaji miti na kuongeza kuwa miti ina nafasi ya kipikee kwa maisha ya watu na kusistiza kuwa bila miti hakuna maisha.

 Ndugai alisema ukataji miti holela ni moja kati ya sababu za mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yamesababisha changamoto nyingi zinazomkabili binadamu ikiwa ni pamoja na athari kwenye uzalishaji wa chakula, upatikanaji wa maji, afya ya viumbe mbali mbali ikiwa ni pamoja na binadamu

 Ni matumaini yangu kuwa zozei hili la upandaji miti litawavuta wakazi wengi wa Kongwa na maeneo mengine nchini kupanda miti kila wanapopata fursa. Pia napenda kuzikumbusha taasisi na makampuni mbali mbali kufikiria juu ya dunia yetu na kuchukua hatua za kuilinda na kuitunza,” alisema


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti akipanda mti huku akishuhudiwa na Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai (aliyevaa kofia) pamoja na wananchi na watumishi wa Halmashauri ya Willaya ya Kongwa mkoani Dodoma. Zoezi hilo la upandaji miti lililofadhiliwa na Kampuni ya Serengeti ikiwa ni sehemu ya jitahada zake za kusaidia utunzaji mazingira.

Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai akimwagilia mti alioupanda wakati wa zoezi la upandaji miti katika wilaya ya Kongwa liliofadhiliwa na kampuni ya Bia ya Serengeti. Wanaoshuhudia ni wanachi na watumishi wa Halmashauri ya wila ya Kongwa.

Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai (kushoto) akiwahutubia wananchi wa wilaya ya Kongwa muda mfupi kabla ya kuanza kwa zoezi la kupanda miti ililifadhiliwa na kampuni ya bia ya Serengeti mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Mark Ocitti

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...