Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
BAADHI
ya wakazi wa mtaa wa Kitende na Kwamfipa wilayani Kibaha ,mkoani Pwani
,wameondokana na kero ya kutembea wakati mwingine kutumia gharama za
usafiri ,kufuata huduma ya afya mbali, baada ya kujengwa kituo cha afya
cha Kibaha specialized polyclinic (KSP),ambacho kimekuwa mkombozi kwao.
Katika
kipindi cha nyuma wakazi hao walikuwa wakitaabika kwenda kituo cha
Mwendapole ,na wakati mwingine hospital ya rufaa ya Tumbi kutokana na
ukosefu wa zahanati na kituo cha afya katika eneo hilo hususan vya
serikali.
Akizungumzia
changamoto za kiafya wakati wa ufunguzi wa kituo cha afya cha KSP
,mkazi wa Kwamfipa bibi Mariam Shomari (77),yeye alisema ,wazee na
watoto walipata shida nyakati hasa za usiku kufuata huduma ya afya
Mwendapole ambapo ni umbali wa km mbili kwenda na kurudi ama kutumia
mabasi madogo ya abiria na pikipiki.
"Tunapata
shida ,mimi ni mzee,nasumbuliwa na ugonjwa wa moyo ,moyo wangu ni
mkubwa ,nalazimika nauli kila wiki kufuata huduma Tumbi ambako zaidi
,pesa sina na watoto wangu wanagharamika sana ,nadhani kungekuwepo
hospital ya serikali tungepata ahueni"
Bibi
Mariam aliiomba serikali, iangalie namna ya kusogeza huduma kwa
kuwajengea zahanati huku wakiendelea kutumia vituo vya watu binafsi
ambavyo kwasasa ndio mkombozi kwao.
Mwenyekiti
wa mtaa wa Kitende, Mchello Mintanga alieleza ,awali kulikuwa na
changamoto ya ukosefu wa dawa kwenye zahanati zilizo karibu nao na
kufuata huduma za kiafya umbali mrefu ambazo kwasasa zimebakia historia
licha ya mahitaji ya zahanati ama kituo cha afya cha serikali.
Kwa
upande wake ,mkurugenzi mkuu wa kituo cha afya cha KSP ,mphamasia
Stephen Stephen alisema ,ameguswa kujenga kituo hicho ili kuwakomboa
wananchi wa maeneo hayo na kuunga mkono juhudi za serikali katika sekta
ya afya ya kusogeza huduma karibu na wananchi.
"Rais
wetu John Magufuli anaipambania sekta ya afya kupunguza changamoto za
miundombinu ,dawa,vifaa tiba hivyo wadau ni wajibu wetu kushirikiana nae
kutatua changamoto hizo " alielezea Stephen.
Stephen
anasema, kituo cha afya KSP ,kinatoa huduma masaa 24 ambapo katika
ufunguzi huo wametoa huduma bure ya kupima shinikizo la damu,uwiano wa
uzito na urefu,uchunguzi wa saratani ya matiti,upimaji wa virusi vya
ukimwi,upimaji wa tezi dume,homa ya ini ,na wametoa elimu ya kujikinga
na magonjwa ya mlipuko.
Mganga
mfawidhi wa KSP Dokta Emmanuel Mniko aliongeza kwamba,kwa siku
wanapokea wagonjwa mbalimbali kutoka maeneo jirani ,wanapokea wenye
majanga ya ajali ,magonjwa ya dharura na kwa mwezi wanapokea wagonjwa
zaidi ya 1,500.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...