Na Jusline Marco-Arusha
Wanawake wajasiriamali Mkoani Arusha wametakiwa kuchangamkia fursa za kimaendeleo kwa kuweka akiba katika banki ya CRDB kupitia akaunti ya malkia kwa maendeleo ya kukuza kipato chao.
Akuzungumza katika hafla ya tuzo ya mwanamke iliyofanyika jijini Arusha,Afisa mikopo CRDB Kanda ya Kaskazini,Emanuel Kafui amesema akaunti hiyo ipo kwa ajili ya kumuwezesha mwanamke kiuchumi kwa kuweka akiba na kupata mikopo.
Kafui amesema kuwa akaunti hiyo inatoa fursa kwa wanawake kipata mikopo kuanzia kiwangi cha shilingi laki tano hadi bilioni tatu ambapo kutia tuzo hizo wana wawezesha wanawake kutambua mchango wao katika kuongeza uchumi.
"CRDB kama Benki ya Kitanzania na mdau muhimu wa maendeleo ya wanaeake katika jamii yetu tumekuja hapa kushiriki tukio hilo ili kumuwezesha mwanamke kutambua juhudi zake katika kujikwamuwa kiuchumi."alisema Kafui
Kwa upande wake mgeni rasmi katika hafla hiyo,Mkurugenzi wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO Mkoa wa Arusha Bi.Nina Nchimbi amesema kuwa mwanamke anapaswa kupambana na changamoto zinazoikabili familia yake kwa kujituma katika shughuli mbalimbali zinazo muingizia kipato na kujutambua.
"Anza kuona ni namna gani wewe kama mwanamke unaweza unaweza ukajikwamuwa kwa kujikubali na kujitambua ili kuweza kufikia maendeleo kwa kuzitatua changamoto hizo"alisisitiza Bi.Nina
Pomoja na hayo amewataka wanawake hao kuishi maisha ya uhalisia na wasiishi maisha ya maigizo kwani kwa kuishi maisha yasiyo halisi kuna uwezekano mkubwa wa kuibomoa familia isiweze kufikia malengo ya kiuchumi na kimaendeleo hivyo amewataka kutambua mabadiliko yoyote yanaanza na mwanamke kwa kujitambua.
Vilevile Bi.Nina ameeleza kuwa katika nyakati hizi mzazi wa kike amemsahau mtoto wa kiume kuliko wa kike katika malezi hali inayosababisha vijana wengi kujiingiza katika kamkundi yasiyofaa hivyo amewataka wananwake kuona kuwa katika jamii waweze kuona wanaenda sawa kwa mtoto wa kike na mtoto wa kiume kwenye utoaji wa malezi ili kuweza kutengeneza jamii iliyobora.
Awali akisoma risala kwa niaba ya muandaaji wa halfla ya mwanamke tuzo,Mkurugenzi wa taasisi ya Noe Movers Bi.Naomi Mrutu amesema kuwa kutokana na changamoto za kila siku kuweza kusababisha migogoro kwenye shughuli za kijasiriamali kampuni ya Fide imwweza kuandaa tuzo hizo ili kuweza kuwasaidia wanawake wa Mkoa wa Arusha kupata ufahamu zaidi juu ya kukabiliana na changamoto hizo katika shughuli zao za kijasiriamali za kila siku.
Ameeleza kuwa kupitia serilikali inayokngozwa na Rais Dkt.John Magufuli imeweza kuwawezesha wanawake kuingia katika masoko kwa njia ya kuvitambua viwanda vidogovidogo na kutoa fursa mbalimbali za uwezeshaji kifedha,kielimu na kiuongozi ambapo taasisi hiyo inaunga mkono jitihada hizo kwa kuwapongeza na kuwatambuwa wanawake wajasiriamali mbalimbali kwa kuwapa tuzo kupitia tamasha hilo chini ya usimamizi wa Baraza la sanaa Tanzania(BASATA).
Naye mmoja wa wajasiriamali katika hafla hiyo Dkt.Petronila Mmasi,Mkurugenzi wa taasisi ya Noela Afya amesema kuwa shughuli yoyote ili ifanyike kwa ufasaha na kuleta chachu ya mabadiliko katika jamii,mjasiriamali anapaswa kuwa na afya njema na imara ambapo taasisi yake inatoa huduma za kiafya kwa wanawake na wanaume hususanj kwenye magojwa ya uzazi na magonjwa yote yakuambukiza na yasiyo ya kuambukiza ikiwemo ugonjwa wa sukari,presha na HIV.
Hata hivyo ugawaji wa tuzo hizo ulizingatia kanuni na vigezo vyote ambapo zoezi hilo liliendeshwa na mwakilishi kutoka Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA)
Afisa mikopo kutoka Banki ya CRDB,Kanda ya Kaskazini ndg.Emmanuel Ikundaeli Kafui akizungumzia huduma zinazotolewa na banki hiyo katika hafla ya ugawaji wa mwanamke tuzo iluuofanyika jijini Arusha.
Katika picha ni mmoja wa washiriki wa mwanamke tuzo ambaye ni mjasiriamali na Mkurugenzi wa taasisi ya Noela Afya Dkt.Petronila Mmasi.
Kulia ni mwenyekiti wa wanawake UWT Mkoa wa Arusha Bi.Yasmin Bachu na katikati ni muandaaji wa tamasha la mwanamke tuzo Bi.Phidesia Mwakitalima,Kushoto ni mkutugenzi wa shule za Upendo Friends Bi.Isabela Mwampamba wakiwa kwenye picha ya pamoja katika tamasha la ugawaji wa mwanamke tuzo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...