
MIRADI 11 kati ya miradi 13 ya maji iliyokuwa inafanywa na wakandarasi yenye thamani ya Sh 6,144,180,650 mkoani Tanga imekamilika kwa asilimia 100 na wananchi wa maeneo ya miradi wapatao 89,484 wanaendelea kupata huduma ya maji.
Miradi hiyo ni miongoni mwa miradi 25 ya maji yenye thamani ya Sh 14,574,399,400 iliyopewa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) na Wizara ya Maji kuisimamia ujenzi wake ili kuboresha huduma ya maji katika miji mbalimbali ya wilaya za mkoani Tanga. Miji hiyo ni Tanga, Muheza, Lushoto, Mkinga, Pangani, Songea, Handeni na Mombo.
Wizara ya Maji ilitoa maagizo hayo kupitia barua yake yenye kumbukumbu namba GC484/379/01B/40 ya Desemba 8,2016 ikiiagiza Tanga UWASA kusimamia miradi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Tanga Uwasa kuelekea maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani inayoanza Machi 16 na kufikia kilele Machi 22, miradi 12 kati ya miradi yote 25 yenye thamani ya Sh 4,216,065,650 inafanywa kwa uwezo wa ndani (Force Account). Miradi hii inatekelezwa kwa ushirikiano na ofisi ya Wakala wa usambazaji majisafi na usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) katika wilaya za Pangani, Mkinga, Muheza na Handeni.
Wakitumia vyanzo vya maji katika miji ya huduma ni Mto Zigi uliojengewa Bwawa la Mabayani lililopo Pande umbali wa kilomita 26 kutoka Tanga Mjini, Mto Mkurumuzi wenye kidakio kilichojengwa katika milima ya Magoroto pamoja na visima nane (8) vilivyopo katika miji yote ya Tanga, Pangani na Muheza,upatikanaji wa maji umefikia wastani wa 83% ya wakazi wote ambapo Tanga ni 89.81%, Pangani ni 69% na Muheza ni34%. Ambapo mtandao wa mabomba ya Majisafi sasa ina urefu wa kilomita 827.37, ambapo kilomita 718.170 ni za Jiji la Tanga, kilomita 65 Pangani na kilomita 44.2 Muheza.
Mamlaka ya hiyo ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) inahudumia wakazi wapatao 371,748 waliomo ndani ya eneo la huduma yaani kata 27 Jijini Tanga, kata 6 Wilaya ya Muheza na kata 4- za wilaya ya Pangani.
Huduma ya uondoshaji wa Majitaka inatekelezwa na Tanga UWASA katika maeneo yake ya kihuduma kwa kupitia mtandao wa mabomba kwa eneo la Jiji la Tanga tu kwa wakazi wapatao 23,391 sawa na asilimia 7.4.
Aidha mradi wa maji wa Muheza ulioanza kutekelezwa mwaka 2019 na kutarajiwa kukamilika mwezi huu kwa gharama za Sh bil 6.3 ukitarajiwa kunufaisha wananchi 15,000 tayari ujenzi wa tangi la kuhifadhia maji la lita 700,000 pamoja na pump house eneo la kilapula kazi imeshajkamilika. Kazi inayoendelea sasa ni ulazaji wa bomba kubwa la kusafirisha maji lenye urefu wa kilomita 8.2 kutoka Mowe - Pongwe – Kilapula – Mkanyageni – Kitisa – Muheza.
Tanga UWASA pia wanasimamia mradi wa kuboresha huduma za maji jiji Tanga, awamu ya pili wenye thamani ya Sh bilioni 8.4 unatarajiwa kuanza mwezi ujao na na kukamilika Desemba mwaka huu. Fedha hizo ni msaada kutoka Benki ya TIB.
Mradi huo unatarajiwa kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji safi kwa saa 24 kwa wakazi wa jijini Tanga na mji wa Muheza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...