NA BALTAZAR MASHAKA, Mwanza

SERIKALI imesema kuwa inathamini misaada ya kijamii inayotolewa na The Desk & Chair Foundation (TD & CF),katika kuunga mkono juhudi za kuwahudumia wananchi wakiwemo wnye mahitaji maalum.

Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dk. Severine Lalika alisema juzi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela, kwenye Maadhismisho ya Siku ya Wanawake Duniani,wakati akipokea msaada wa vifaa vya kujifungulia akinamama na baiskeli za walemavu.

Alisema serikali kwa namna ya pekee inaishukuru TD & CF kwa kuunga mkono juhudi zake za kuhakikisha Watanzania wenye mahitaji maalum nao wananufaika na wanajisikia faraja kwa kupata huduma za kijamii kama hizo.

“Nikuhakikishie kwa misaada mnayotoa kama ujenzi wa vyoo kwa shule zetu za msingi na baadhi ya shule za sekondari,serikali tunaithamini sana misaada ya namna hiyo,”alisema Dk. Lalika.

Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation, Tawi la Tanzania, Alhaji Sibtain Meghjee,alisema msaada huo wa vifaa mifuko 184 kwa ajili ya akinamama wakati wa kujifungua na baiskeli mbili za watu wenye ulemavu umegharimu sh.milioni 6.7.

Alisema walifanya utafiti wao wakabaini akina mama wajawazito wana changamoto ya kukosa vifaa wanapokwenda kujifungua na baada ya kuguswa na changamoto hiyo mwaka huu kwenye madhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wameamua kutoa mifuko 184 yenye thamani ya sh.milioni 5.55 vigawiwe bure ambapo mwaka jana waligawa mifuko 280.

Pia baiskeli mbili kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye walemavu zenye thamani ya sh.milioni 1.2 na kufanya idadi ya vyenzo hizo zilizotolewa bure kwa watu hao wenye mahitaji maalum kufikia jumla ya baiskeli 569.

Alhaji Meghjee alisema taasisi hiyo yenye makao makuu nchini Uingereza ilianzishwa mwaka 2003 na Watanzania wenye asili ya Kiasia (wote wazaliwa wa Mwanza) na kwa Tanzania ilisajiliwa na kuanza kazi mwaka 2004.

“Taasisi hii tulianzisha mwaka 2003 ili kusaidia jamii na waalinzishi wote ni wazaliwa wa hapa Mwanza na tunafanya kazi bila kubagua kwa kusaidia jamii katika sekta za afya, elimu na maji,”alisema

Aidha alhaji Meghjee alieleza kuwa taasisi hiyo inajishughulisha na utoaji wa misaada ya kijamii ikigharamia baadhi ya matibabu ya wagonjwa,ujenzi wa vyoo,madarasa,sare za shule na utengenezaji wa madawati. Pia imechimba visima vifupi na virefu vya maji hasa maeneo ya vijijini na kwenye baadhi ya taasisi za umma pamoja na kutoa vifaa mbalimbali saidizi kwa watu wenye mahitaji maalum.


Gari la taasisi ya The Desk & Chair Foundation (TD & CF) lenye namba T 989 CHV likiwa limebeba vifaa mbalimbali vilivyotolewa bure na taasisi hiyo ili kuwasaidia akina mama wajawazito wakati wa kujifungua.

Vifaa hivyo ni ufadhili ama sadaka kwa ajili ya kumbukumbu ya marehemu Gulam Hussein Bandali Damji.Picha zote na Baltazar Mashaka

Mifuko yenye vifaa hivyo vilivyogharimu sh.5,550,000 kama inavyoonekana.

Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation (TD & CF),Tawi la Tanzania, Alhaji Sibtain Meghjee (kushoto), akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dk.Severine Lalika kuhusu baiskeli mbili za walemavu kabla ya kumkabidhi juzi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.Basikeli hizo za kisasa zimegharimu sh. milioni 1.2.

 
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dk.Severine Lalika (kulia) akipokea moja ya mifuko 184 ya vifaa vya wajawazito kutoka kwa Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation (TD & CF), Alhaji Sibtain Meghjee juzi, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa wilayania Ilemela.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...