Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Na Mwandishi Wetu
SSERIKALI imewaasa wafungwa wote nchini kuzidisha kufanya ibada sambamba na kuzidisha kumuomba mungu ili wakitoka waende kuwa raia wema Pamoja na kukamilisha ndoto zao walizokua nazo
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Khamis Hamza Chilo katika kikao kikao cha ndani kilichohusisha wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Sindida mjini ambapo pia alipata fursa ya kuwasikiliza wafungwa ambao walitoa maoni,mapendekezo na changamoto mbalimbali walizokua nazo ikiwemo kuchelewa kwa upepelezi wa kesi zao.
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawategemea sana hasa vijana na Taifa hili linawategemea sana,hapa naona vijana mko wengi vijana ndio nguvu kazi ya Taifa,sasa endeleeni kuwa raia wema,ukitoka hapa kifungoni nenda kawe raia mwema,mkitoka hapa nendeni mkaendeleze ndoto zenu,fanyeni ibada muombeni mungu sana fanyeni ibada huwezi kujua ukitoka hapa utaenda kuwa nani maana historia inatuonyesha wako watu mbalimbali walikua wafungwa lakini walivyomaliza vifungo vyao walienda kuwa viongozi wakubwa tu.” Alisema Naibu Waziri Chilo
Akisoma taarifa ya gereza mbele ya Naibu Waziri, Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Singida, amesema katika gereza hilo kuna shughuli mbalimbali za uzalishaji ikiwemo kilimo cha mahindi,maharage,kilimo cha mbogamboga,ufyatuaji wa tofali,ufugaji wa Samaki,ujenzi wa nyumba za makazi ya askari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...