SERIKALI imezindua Umoja wa Wadau wa Ubora kitaifa Tanzania (NQAT), utakaotumika kama jukwaa la kuwasaidia wazalishaji wa bidhaa mbali mbali kutoka sekta binafsi na Umma kukaa pamoja na kubadilishana mawazo mbalimbali katika tasnia ya ubora.

Aidha utasaidia kuzalisha na kutoa huduma za kiushindani katika soko la kimataifa,

Umoja huo umezinduliwa na Naibu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dkt. Emmanuel Munisi hivi karibu kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara uliyoandaliwa na Mradi wa Kuwasaidia Wakulima Kuongeza Thamani ya Mazao na namna ya kufikia Masoko (MARKUP), uliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa maktaba wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Amesema, umoja huo utawaleta wataalamu, wadau, washirika pamoja, ambapo kutakuwa na upana mkubwa wa historia na uzoefu ambao watabadilishana, kuhakikisha utamaduni bora na mawazo bora yanaingia kwenye jamii yetu huku pia umoja huo ukichukua nafasi ya kusema mfumo bora wa miundombinu ambayo ni moja ya hatua chanya na vitendo, ambapo ni njia ya kuunda uchumi unaostawi kama msingi wa kustawi afya na hali nzuri.

"Mfumo mzuri na bora wa miundombinu huchangia katika sera na malengo ya Serikali kufika Maendeleo ya viwanda, ushindani wa kibiashara kwenye Soko la dunia, ufanisi katika utumiaji wa rasilimali asilia na rasilimali watu, usalama wa chakula, afya , mazingira na pia mabadiliko ya tabia nchi amesema.

Naye, Mratibu wa mradi wa kusaidia wajasiliamali Tanzania katika kuongeza thamani kwenye bidhaa na huduma(MARKUP), Safari Fungo amesema hatua hiyo imeweka historia na itasaidia kuchagiza katika kukuza zaidi uchumi wa nchi.

"Kuzinduliwa kwa umoja huo wa Wadau wa Ubora nchini ni matokeo ya mradi wetu wa Markup, "tunafahamu kwamba ubora upo kwenye huduma, bidhaa na kwenye kila kitu, kwa hiyo umoja huu utakuwa unakutanisha wadau kutoka katika sekta mbalimbali kuzungumzia fursa, changamoto na kupashana habari za maendeleo katika sekta hiyo kwa ajili ya kushindana katika soko la kimataifa.” Amesema Fungo.

Amesema wazalishaji wengi wa bidhaa na watoa huduma, wamekuwa wakipata changamoto kubwa kwenye ushindani katika soko la kimataifa kutokana na kukosekana kwa jukwaa la kujadili namna ya kutatua matatizo yaliyopo katika sekta hiyo na kuyatafutia ufumbuzi.

“Kumekuwepo kwa baadhi ya changamoto lakini hakuna majawabu na hivyo kusababisha kukosekana kwa matokeo mazuri katika sekta hiyo ya kutoa huduma zenye ubora hasa katika suala la kushindana kimataifa, majukwaa kama haya yapo katika sekta mbalimbali ikiwamo za uhandisi, Udaktari, Ualimu, na huku tumeona liwapo ili kuchochea maendeleo endelevu ya nchi yetu.”

Ameongeza kuwa jukwaa hilo pia itachochea maendeleo kwa wajasiliamali wengi kujifunza mambo mengi na kuwasaidia kutoka katika hatua moja kwende nyingine.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa Umoja huo, Amily Hamza, ameema kupatikana kwa usajili wa umoja huo kutasaidia kupandisha zaidi uchumi wa nchi kwa sababu matatizo mengi yaliyopo kwa sasa yatakuwa yanapatiwa ufumbuzi kwa haraka zaidi.

Kupitia umoja wetu huu, Uchumi wa nchi utapanda juu, viwanda vyetu vitaweza kupeleka bidhaa nje na pia kushindana kwa kuzalisha bidhaa ambazo zitakuwazinaingia nchi za nje , kwa hiyo uchumi wa Tanzania utainuka, Tanzania ya viwanda itakuwa sio ndogo tena," amesema Hamza.

Amesema changamoto walizokutana nazo mwanzo ni namna ya kuanzisha umoja huo kama waende Brela au wapi, lakini baada ya kupitia kwa wataalamu wa sheria wakapata usajali Brela na faida itakayipatikana haitaingia katika mifuko yetu bali itasaidia viwanda vidogo.

“Tunaamini kwa kupata kibali hiki cha kuanzisha umoja huu, viwanda vitazalisha bidhaa nyingi zenye ubora ambao utakidhi vigezo vya kimataifa na chumi wa nchi utapanda zaidi kwa sababu viwanda vitapeleka bidhaa nje ya nchi kwa wingi kushindana katika soko la kimataifa na Tanzania ya viwanda itakuwa ni ya Uhakika zaidi.” Alisema Hamza.

Naibu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dkt. Emmanuel Munisi, Mratibu wa mradi wa kusaidia wajasiliamali Tanzania katika kuongeza thamani kwenye bidhaa na huduma(MARKUP), Safari Fungo wakiwa katika picha ya pamoja.
Naibu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dkt. Emmanuel Munisi akizungumza wakati wa kuzindua Umoja wa Wadau wa Ubora kitaifa Tanzania (NQAT), utakaotumika kama jukwaa la kuwasaidia wazalishaji wa bidhaa mbali mbali kutoka sekta binafsi na Umma kukaa pamoja na kubadilishana mawazo mbalimbali.

Mratibu wa mradi wa kusaidia wajasiliamali Tanzania katika kuongeza thamani kwenye bidhaa na huduma(MARKUP), Safari Fungo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Wadau wa Ubora kitaifa Tanzania (NQAT), utakaotumika kama jukwaa la kuwasaidia wazalishaji wa bidhaa mbali mbali kutoka sekta binafsi na Umma kukaa pamoja na kubadilishana mawazo mbalimbali.
Baadhi ya wadau wakitoa maada katika Mkutano uliofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.





Baadhi ya washiriki wa mkutano wakisikiliza mada.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...