Jane Edward,Michuzi TV,Arusha

Wafanyabiashara mbalimbali mkoani Arusha wamemlilia Hayati Rais John Pombe Magufuli kwa namna ambavyo aliweka nidhamu kwenye biashara na kuendelea kuwapa moyo wafanyabiashara mbalimbali kuchangia Kodi kutokana na utendaji kazi mzuri aliokuwa nayo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wafanyabiashara hao, Mkurugenzi wa makampuni ya Benson yaliyopo mkoani Arusha Naushad Hussein alisema kuwa,kifo Cha Rais Magufuli ni pigo kubwa kwa nchi yetu kutokana na jinsi alivyoitengeneza nchi kwa kipindi cha miaka mitano tu.

Alisema kuwa,Rais Magufuli atakumbukwa kwa mengi sana ambayo ameyafanya ikiwemo kuweka nidhamu ya biashara ambayo imewafanya wafanyabiashara mbalimbali kulipa Kodi kwa uhakika kutoka na kazi zinazoonekana.

Naye  Meneja wa Tanroad mkoani Arusha,Injinia John Kalupale alisema kuwa,kwa kweli nchi imepata pigo kubwa sana na ni msiba wa kitaifa ambao hauzoeleki kwani alikuwa mtu ambaye hakubagua mtu yeyote dini au kabila alitenda haki kwa watanzania wote
.

Mfanyabiashara Naushad Hussein, Akizungumza na vyombo vya Habari ofisini kwake Jijini Arusha, juu ya msiba wa Hayati John Pombe Magufuli (Picha na Jane Edward, Michuzi TV, Àrusha).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...