Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amewahimiza Watumishi wa Wizara kufanya kazi kwa kujituma, weledi na nidhamu. Amesema haya alipokuwa akifungua mafunzo maalumu ya siku tano kwa Watumishi wa Wizara yanayoendelea jijini Dodoma.
Katibu
Mkuu amewakumbusha na kusisitiza kuwa, Watumishi wa Wizara wakati wote
wakiwa katika utekelezaji wa majumu yao iwe ndani au nje ya mipaka ya
nchi, wanapaswa kuielewa na kuzingatia miongozo mbalimbali inayotumiwa
na Wizara. Ameitaja baadhi ya miongozo hiyo kuwa ni pamoja na Sera ya
Mambo ya Nje, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Ilani ya CCM ya Mwaka
2020-2025, Hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
wakati anafungua Bunge la 12, Mpango Mkakati wa Wizara ambao huhuishwa
kila mwaka wa fedha, na sheria na kanuni zinazoongoza utumishi nje.
Aliongeza kuwa Mkataba wa Vienna (Vienna Convention) wa Mwaka 1961 na
ule wa mwaka 1963 unaohusu mahusiano ya kidiplomasia na mahusiano ya
kikonseli mtawalia pamoja na Kanuni za Utumishi Nje za Mwaka 2016 pia ni
muhimu zizingatiwe.
“Natambua
ni ndoto ya kila Afisa Mambo ya Nje (Foreign Service Officer) ni kwenda
posting siku moja, kwa mtakaobahatika kupata fursa ya kwenda kwenye
Balozi zetu, mjue kwamba mna deni kubwa kwa nchi yenu. Mnawiwa
kutekeleza majukumu yenu kwa kujituma, uzalendo, na kuhakikisha ulinzi
na usalama wa maslahi ya nchi yetu.” Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A.
Ibuge.
Licha
ya mafunzo hayo kulenga kuwasaidia watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuelewa misingi bora ya maadili ndani
ya Utumishi wa Umma, Balozi Brigedia Jenerali Ibuge ameeleza mataumani
yake kuwa mafunzo hayo yatawasaidia watumishi kupata uelewa wa jumla
kuhusu Maslahi ya Taifa, Diplomasia ya Uchumi, Itifaki, Usalama wa
kimtandao na utendaji wa kazi katika mazingira ya kimataifa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge akizungumza na Watumishi wa Wizara (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalumu kwa watumishi hao yatakayofanyika katika ukumbi wa Veta, jijini Dodoma. |
Shemu nyingine ya Watumishi wa Wizara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Mafunzo |
Shemu nyingine ya Watumishi wa Wizara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Mafunzo |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...