NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MKOA
wa Pwani ,umepitisha rasimu ya mapendekezo ya mpango na bajeti wa mwaka
2021/2022 ,ya kiasi cha sh.bilioni 298 ikiwa ni ongezeko la sh .bilioni
25 sawa na asilimia 9 kutoka katika bajeti ya mwaka 2020-2021 ya
sh.bilioni 272.
Kufuatia
ongezeko hilo ,sekretarieti ya mkoa imezisihi halmashauri za wilaya na
mji kuongeza nguvu ya ukusanyaji wa mapato pamoja na kutafuta vyanzo
vipya vya mapato ya ndani.
Akiwasilisha
rasimu hiyo ya mapendekezo ,kwenye kikao cha ushauri cha mkoa wa Pwani
(RCC),Mchumi wa mkoa huo Gerald Mbosoli alisema, zipo halmashauri ambazo
hazijafikia asilimia 50 hadi kufikia Desemba mwaka jana hivyo anaamini
kufikia June mwaka huu malengo yatafikiwa.
"Ila
katika utekelezaji wa bejeti inayomalizika kulikuwa na changamoto ya
upungufu wa vitendea kazi ,watumishi na raslimali fedha hazitoshelezi
kulingana na uhalisia." alielezea Mbosoli.
Mbosoli alieleza, ipo mikakati waliyojiwekea ikiwa ni pamoja na uboreshaji katika huduma za jamii na kusanyaji wa mapato .
Alifafanua
kwamba, maeneo mengine ni usimamizi wa stahiki za wananchi na maeneo
yaliyopewa vipaombele na ni mtambuka ikiwemo VVU ,lishe .
Akifunga
kikao hicho mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo alizitaka
halmashauri kuongeza juhudi za kusimamia makusanyo na kufuatilia mianya
ya upotevu wa mapato ili kuinua mapato yao.
Akizungumzia
hoja iliyoibuka kutoka wilaya ya Mafia juu ya mapato makubwa kuelekea
jiji la Ilala ,alisema baharini hakuna vizuia ,lakini zipo halmashauri
zinazoumia kutokana na sheria zilizopo.
Akichangia
agenda hiyo, mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mafia ,Erick
Mapunda alisema kuwa wana changamoto kubwa ya mapato ya wavuvi wadogo
kulipiwa jiji la Ilala.
"Wapo
wavuvi wadogo kutoka Dar es salaam ambao wamekuja Mafia na kutumia eneo
letu kuvua na kuondoka kujipatia soko Dar es salaam ,hawa wamekuwa
wakikataa kulipia ,hali inayosababisha halmashauri yetu kukosa mapato
makubwa kutoka kwao ,"
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...