NA YEREMIAS NGERANGERA….NAMTUMBO.
Akichangia mapendekezo ya bajeti 2021/2022 ya Halmashauri ya wilaya Namtumbo diwani wa kata ya likuyu wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma bwana Kassimu Gunda alisema anaiomba serikali kuwaingiza wazee waliotelekezwa na watoto wao ambao wanafanyakazi za serikali au katika taasisi binafsi kwa kuwa wanamazingira magumu na wanastahili kunufaika na mfuko wa kunusuru kaya maskini TASAF.
Gunda alidai ruzuku ya miradi ya maendeleo kutoka kwa wadau wa maendeleo ikiwemo ya TASAF anaiomba serikali ruzuku hiyo iangalie watu wanaoishi katika mazingira magumu bila kujali baadhi ya wazazi wana watoto wenye nafasi kubwa serikali huku watoto hao wamewatelekeza wazazi wao na wanaishi katika mazingira magumu na wanahaki ya kunufaika na mpango wa TASAF.
Aidha bwana gunda alisema kuna mifano dhahiri kuwa wapo wafanyakazi wa serikali wakishaoa na kuwa na familia huwatelekeza wazazi wao ingawa sio wote lakini wapo na katika mazingira hayo wazazi wa familia hizo waingizwe katika mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF na sio kuwaacha kwa kigezo cha kuwa na watoto wanaofanya kazi ambao hawawahudumii wazazi wao.
Naye diwani wa kata ya Mkongo Daniel Nyambo alisema katika kutengeneza bajeti ya 2021/2022 Halmashauri ihakikishe inajikita katika kuimarisha mfuko wa CHF iliyoboreshwa ili makusanyo watakayopatikana yaweze kutoa huduma bora za afya katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Awali afisa mipango wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo bwana Amos Kanige alisema Halmashauri kupitia ruzuku ya maendeleo inatarajia kuboresha huduma kwa wananchi kwa kuweka mazingira wezeshi ya utoaji ruzuku ya fedha ya kunusuru kaya maskini TASAF .
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Namtumbo bwana Juma Pandu aliwata watumishi wa serikali kuongeza ufanisi wa kazi ,kuongeza ushirikiano kati yao na waheshimiwa madiwani pamoja na wananchi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo.
Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo limepitisha mapendekezo ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwa kukisia kukusanya na kupokea jumla ya 28,237,660,400 huku ikikisia kutumia 18,043,444,000 kwa ajili ya mishahara, Tsh 7,335,523,,400 kwa ajili miradi ya maendeleo na Tsh 2,858,693,000 kwa ajili ya matumizi mengineyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...