


*****************************************
Wajumbe wa mkutano
mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Hanang’ Mkoani Manyara, wametimiza kiu
yao kubwa ya kumpata mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo baada ya kusubiri
kwa miaka kadhaa sasa.
Akizungumza wakati wa
kufunguo mkutano huo mkuu wa Uvccm Hanang, Mgeni rasmi ambae pia ni
Mbunge wa Jimbo la Hanang Ndugu Samwel Hhayuma Xaday ameendelea
kuwambusha vijana wote juu ya Umuhimu wa kumchagua kiongozi wa Vijana
anayetokana na Vijana wenyewe atakaebeba maono na matamanio ya vijana
wote bila kuyumbishwa kwani kwa kufanya hivo mtakua mmepata sauti yenu
katika vikao mbalimbali vya maamuzi na kuwainua vijana wengi zaidi
kufikia ndoto zao.
“Ninaomba baada ya
kukamilika kwa uchaguzi huu mwenyekiti atakayepatikana anipe mpango kazi
wenu ili nijue namimi nashiriki vipi kukamilisha ndoto na matarajio
yenu mliojiwekea. Hamasa ya vijana, michezo na ajira kwa vijana wetu
bado sio ya kuridhisha sana” aliongeza Mh Hhayuma.
Wagombea katika uchaguzi kwa nafasi mwenyekiti na kura walizopata ni kama Ifuatavyo.
1.Angel Nicolaus 19
2.Desderi Dismas 32
3.Elifido Daffi 10
4.Eng Timoth Caroly 4
5.Joseph Ginawe 61
6.Masweti Africanus 5
7.Yohani Leonce 262
Baada ya msimamizi wa
uchaguzi kumtangaza mshindi ndugu Yohani Leonce amewashukuru wajumbe
wote na kuwaahidi kuendelea pale tulipoishia ikiwa ni pamoja na
Kuhakikisha upatikanaji wa Jengo la Katibu na Kufufua ari na hamasa kwa
vijana wote kwa kuanza na ziara maalum ya kuwafikia mahali walipo.
“Niwaombe wagombea
wenzangu tushikamane kwa pamoja na yale mawazo yote mliokuwa mnatamani
kila mmoja wetu nitayatekeleza kwa nguvu zangu zote,” amesema Leonce.
Tunawashukuru sana wasimamizi wa Uchaguzi huu katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa Mwl Jacob Siay kwa usimamizi wa uchaguzi uliotuka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...