Katika kuadhimisha siku ya figo duniani ambayo hufanyika Machi 11 kila mwaka, watumishi zaidi 460 wa Hospitali ya Taifa Muhimbili- Upanga wamepima afya ili kubaini kama wana magonjwa ya figo au la.
Lengo la watumishi wa Muhimbili kupimwa afya ni kuwasaidia kujua hali za afya zao mapema kwa kuwa wamekuwa wakienda hospitali katika hatua za mwisho ya magonjwa ya figo.
Akizungumza kuhusu upamaji afya kwa watumishi wa Muhimbili, Dkt. Onesmo Kisanga amesema hatua hiyo itasaidia watumishi kuanza mapema huduma za matibabu endapo uchunguzi utabainisha kama wana magonjwa ya figo.
“Tunapenda kuwapima afya watumishi wetu ili kama wana magonjwa ya figo, waweze kutibiwa mapema na kuendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa,” amesema Dkt. Kisanga.
Amesema upamaji wa afya kwa watumishi unahusisha, kupima kisukari, shinikizo la damu, uzito, mkojo pamoja na kutoa elimu ya afya.
“Watu wengi hawajui kama uzito unasababisha kisukari na shinikizo la damu sasa ili kuwa katika afya nzuri, tunapaswa kuwa makini na afya zetu kwa sababu uchunguzi unasaidia kuzuia uharibifu wa figo,” amesema Dkt. Kisanga.
Dkt. Kisanga amesema faida kubwa ya kupima afya mara kwa mara, inasadia watu kupatiwa matibabu mapema endapo itabainika mtu au watu wana magonjwa figo.
Upimaji afya kwa watumishi, utaendelea wiki ijayo Alhamisi na Ijumaa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila ambako wametakiwa kujitokeza kwa wingi.
Mmoja wa watumishi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Upanga akipimwa afya ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya figo duniani ambayo hufanyika Machi 11 kila mwaka. Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo wa Muhimbili, Dkt. Onesmo Kisanga akizungumza kuhusu upimaji wa magonjwa ya figo kwa watumishi wa Muhimbili.Baadhi ya watumishi wakisubiri kupima vipimo vinavyohusisha uchunguzi wa magonjwa ya figo. Dkt. Kisanga (katikati) akiwa katika picha pamoja na madaktari bingwa wa magonjwa ya figo wa Muhimbili. Kushoto ni Dkt. Jacquline Shoo na Dkt. Muhidin.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...