Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi ,Maliasili na Utalii imeipongeza
Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Shirika la Hifadhi za Taifa
(TANAPA) kwa kupunguza tatizo la ujangili hapa nchini .
Mwenyekiti
wa Kamati hiyo Dkt. Aloyce Kwezi ametoa pongezi wakati wa ziara ya
Kamati hiyo katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na maeneo yanayosimamiwa na
Wakala wa Hudma za Misitu Tanzania (TFS) ambapo amesema hatua hiyo
imesaidia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa idadi ya wanyama.
"Napongeza
kazi kubwa iliyofanywa na Wizara, TANAPA wamefanya kazi kubwa sana ya
kupunguza ujangili, hili limesaidia kuongezeka kwa idadi ya wanyamapori
hapa nchini, pia nawapongeza TFS kwa kazi kubwa ambayo wameifanya"
Amesema Dkt Kwezi
Kuhusu uboreshaji wa miundombinu maeneo ya
Hifadhi, Kamati hiyo imeishauri Wizara katika kipindi hiki cha Bajeti
kufuatilia kwa karibu ujenzi wa Barabara inayotoka Iringa kuelekea
katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha .
"Tunaomba suala hili
lifuatiliwe kwa ukaribu katika kipindi hiki cha bajeti, barabara ya
kuingia katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha bado ina changamoto, lazima
iwekewe nguvu na sisi tuko pamoja na kwenye jambo hili kuhakikisha
limefanikiwa kwa sababu hifadhi hii ina vivutio vizuri sana .
Amesisitiza Dkt. Kwezi
Mwenyekiti huyo amepongeza hatua ya
ununuzi wa mitambo iliopatikana chini ya Mradi wa REGROW ya kufanya
marekebisho na matengenezo ya barabara zilizoko ndani ya hifadhi
akieleza kuwa hatua hiyo inapunguza gharama na kufanya ukarabati uwe
endelevu.
“Nawapongeza kwa hatua hii, mnapokuwa na mitambo yenu
wenyewe mnapunguza gharama na kufanya utengenezaji wa barabara za ndani
ya hifadhi uwe endelevu” Amesema.
Kuhusu utengenezaji wa bidhaa
zitokanazo na mazao ya misitu amesema kuwa Kamati ingependa kuona
tekinolojia ya ubunifu ya kutengeza mkaa mbadala inasambazwa kwenye
maeneo mengi hapa nchini ili wananchi waweze kuitumia kukailiana na
tatizo la matumizi ya mkaa ambao umekua chanzo cha uharibifu wa
Mazingira.
Mbali na hilo amesema takribani hekta 662 zimepotea
kwa moto kichaa na kuisababishia Serikali hasara jambo lililoifanya
Kamati hiyo kutoa maagizo kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani humo
idhibiti matukio hayo kwa kuweka Sheria ambazo zitasaidia kuondoa hasara
hiyo.
Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas
Ndumbaro ameiambia Kamati hiyo kuwa Wizara itayafanyia kazi maelekezo
na ushauri uliotolewa na kamati hiyo.
"Ninawashukuru kwa ziara
hii pamoja na maelekezo mliyoyatoa , kama mnavyofahamu Hifadhi ya ya
Ruaha ina ukubwa wa Kilometa za Mraba 22,000, eneo eneo hili ni kubwa
kuliko hata baadhi ya nchi pia ni kubwa kuliko Mkoa wa Mtwara, na kwa
kiasi kikubwa miundombinu yake sio mizuri hasa upande wa Ruaha kusini,
hili tutalifanyia kazi "Amesema Dkt. Ndumbaro
Naye Naibu Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amesema amepokea ushauri
uliotolewa na kamati hiyo na kuahidi kuufanyia kazi huku akieleza kuwa
barabara inayotoka Iringa kwenda Hifadhi ya Taifa ya Ruaha imeshaanza
kufanyiwa kazi na ipo katika hatua ya upembuzi yakinifu .
"Kwa kuwa tunaelekea kwenye bajeti, barabara hii tutaipa kipaumbele Ili iweze kutengenezwa na kupitika vizuri "
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (katikati) akiiomba kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii isaidie kuhamasisha Utalii wa ndani wakati wa Kikao kifupi cha Majadiliano, Mapendekezo na Maelekezo kilichofanywa na Kamati hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Sao- Hill mkoani Iringa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce A. Kwezi akiipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kazi kubwa inayofanyika ya kulinda, kuendeleza na kuhifadhi Maliasili za nchi wakati wa Kikao kifupi cha majadiliano cha Kamati hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano Sao- Hill mkoani Iringa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...