Na Ankal
Nikiwa na James Mpinga, mmoja wa waandishi wa habari wakongwe na nguli ambaye sifa yake kuu ni ubunifu uliotukuka na unaoacha alama. Hapa ni katika ofisi za Daily News jijini Dar.

James ni mmoja wa role models wangu katika fani hii ya uandishi. Namkumbuka kwa mambo mengi, ikiwa ni pamoja na ucheshi na utani mwingi. Lakini hili la ubunifu namvulia kofia, hasa nikikumbuka siku moja tukiwa chumba cha habari mara tu baada ya Dkt. Ali Mohamed Shein kutangazwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi mara tu baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2010.

Story, picha na kila kitu kilikuwa kimekamilika siku hiyo wakati tunaandaa gazeti la kesho. Tatizo likawa ni kichwa cha habari kipi kitachoendana na habari hiyo kubwa ya kumpata kiongozi mpya wa Zanzibar.

Msanifu Mkuu (anaitwa Chief sub-editor kwa kimombo kama sikosei) siku hiyo alikuwa James Mpinga. Muda wa kupeleka gazeti kuchapwa ulikuwa unakaribia lakini bado kichwa cha habari kwa habari kiongozi (lead story) hiyo kilikuwa bado kupatikana. 

Zikiwa zimesalia dakika tano kabla ya kufunga matayarisho na gazeti kupelekwa mitamboni, James akaibuka kutoka kiti chake na kusema Got it! Yaani keshakipata hicho cha habari. News room yote ikabaki kimya na kumgeukia.

Huku akicheka James Mpinga akasema kichwa cha habari kitakuwa "DR. WHO?"

Hadi leo naikumbuka siku hiyo, hususan kichwa cha habari hiyo, kwani sio tu kilimshangaza na wakati huo huo kumfurahisha kila mmoja wetu na hata wasomaji wa Daily News siku hiyo. Huyo ndiye James Mpinga katika kokwa ya njugu. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...