Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Songea Mjini , Dkt. Damas Ndumbaro akikata utepe wakati akizindua rasmi msimu wa saba wa Tamasha la Majimaji Selebuka litakalofanyika kuanzia tarehe 24 hadi 31 Julai kwenye Viwanja vya Maji Maji Songea mkoani Ruvuma. Wa pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Songea, Mhe. Pololet Mgema akiwa na Viongozi wengine wa Kiserikali na Taasisi za Misitu nchini.
====== ======= =========
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ameziagiza Taasisi zote za
Wizara ya Maliasili na Utalii ambazo zinatangaza Utalii na zinafanya
Uhifadhi kuweza kushiriki Tamasha la Majimaji Selebuka.
Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika mkoani Ruvuma kuanzia
tarehe 24 Julai hadi 31 mwaka huu katika Uwanja wa Majimaji Songea
likiwa na lengo la kuhamasisha utalii wa ndani, michezo pamoja na kukuza
na kuenzi utamaduni wetu.
Ametoa agizo hilo wakati akizindua msimu wa saba la
Tamasha hilo uliofanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia 24 na 25 Aprili
katika Viwanja vya Makumbusho ya Majimaji ikiwa ni maandalizi ya
Tamasha lenyewe litakalofanyika mwezi Julai kwa muda wa siku saba
mkoani hapo.Katika Tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu limebeba kauli
mbiu isemayo ” Misitu ni Uchumi ” Dkt.Ndumbaro amesema kwa mwaka huu
Tamasha linatoa hamasa kwa Jamii kutunza misitu zaidi.
Waziri Dkt. Ndumbaro amesema anategemea Tamasha hilo kwa
mwaka huu litakuwa kubwa sana na litatoa fursa kwa Watu mbalimbali
kuanza kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii ambavyo vipo mkoani
Ruvuma likiwemo Pori la Akiba LipalambaKatika hatua nyingine, Amemuomba Mkuu wa Wilaya ya Songea
kutumia mamlaka yake ya kuzitaka Taasisi zilizo katika wilaya yake
kushiriki katika Tamasha hilo.
‘” Mkuu wa wilaya najua una Taasisi nyingi sana katika
wilaya yako ninakuomba na ninaamini una Mamlaka hiyo, toa maelekzo kwa
Taasisi zote zinanazotoa huduma na kufanya biashara zishiriki Tamasha la
Majimaji Selebuka ” alisisitiza Waziri Dkt.Ndumbaro Aidha amezitaka Halmashauri ya Songea pamoja Halmashauri zingine ziweze kushiriki Tamasha hiloAidha, Waziri Dkt. Ndumbaro ametumia fursa hiyo kuziomba
Taasisi nyingine za Watu binafsi kushiriki katika Tamasha hilo ili
ziweze kutoa huduma kwa jamii katika msimu wa Tamasha hilo.
Kwa upande wake Mratibu wa Tamasha hilo Reinfrida Rwezaura,
amesema Tamasha hilo tangu kuanzishwa kwake limekuwa ni Jukwaa bora kwa
kuwakutanisha Wafanyabiashara, Wajasiliamali, wanamichezo, wanafunzi,
na wadau mbalimbali katika kuendelea kuutangaza uchumi na utalii nchini Waziri wa Maliasili na Utalii,
Dkt.Damas Ndumbaro ameziagiza Taasisi zote za Wizara ya Maliasili na
Utalii ambazo zinatangaza Utalii na zinafanya Uhifadhi kuweza kushiriki
Tamasha la Majimaji Selebuka.
Tamasha hilo linatarajiwa
kufanyika mkoani Ruvuma kuanzia tarehe 24 Julai hadi 31 mwaka huu
katika Uwanja wa Majimaji Songea likiwa na lengo la kuhamasisha utalii
wa ndani, michezo pamoja na kukuza na kuenzi utamaduni wetu.
Ametoa agizo hilo wakati
akizindua msimu wa saba la Tamasha hilo uliofanyika kwa muda wa siku
mbili kuanzia 24 na 25 Aprili katika Viwanja vya Makumbusho ya Majimaji
ikiwa ni maandalizi ya Tamasha lenyewe litakalofanyika mwezi Julai kwa
muda wa siku saba mkoani hapoKatika Tamasha hilo ambalo kwa
mwaka huu limebeba kauli mbiu isemayo ” Misitu ni Uchumi ” Dkt.Ndumbaro
amesema kwa mwaka huu Tamasha linatoa hamasa kwa Jamii kutunza misitu
zaidi.
Waziri Dkt. Ndumbaro amesema
anategemea Tamasha hilo kwa mwaka huu litakuwa kubwa sana na litatoa
fursa kwa Watu mbalimbali kuanza kutembelea vivutio mbalimbali vya
Utalii ambavyo vipo mkoani Ruvuma likiwemo Pori la Akiba LipalambaKatika hatua nyingine, Amemuomba
Mkuu wa Wilaya ya Songea kutumia mamlaka yake ya kuzitaka Taasisi
zilizo katika wilaya yake kushiriki katika Tamasha hilo.
‘” Mkuu wa wilaya najua una
Taasisi nyingi sana katika wilaya yako ninakuomba na ninaamini una
Mamlaka hiyo, toa maelekzo kwa Taasisi zote zinanazotoa huduma na
kufanya biashara zishiriki Tamasha la Majimaji Selebuka ” alisisitiza
Waziri Dkt.Ndumbaro
Aidha amezitaka Halmashauri ya Songea pamoja Halmashauri zingine ziweze kushiriki Tamasha hilo
Aidha, Waziri Dkt. Ndumbaro
ametumia fursa hiyo kuziomba Taasisi nyingine za Watu binafsi kushiriki
katika Tamasha hilo ili ziweze kutoa huduma kwa jamii katika msimu wa
Tamasha hilo.Kwa upande wake Mratibu wa
Tamasha hilo Reinfrida Rwezaura, amesema Tamasha hilo tangu kuanzishwa
kwake limekuwa ni Jukwaa bora kwa kuwakutanisha Wafanyabiashara,
Wajasiliamali, wanamichezo, wanafunzi, na wadau mbalimbali katika
kuendelea kuutangaza uchumi na utalii nchini
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...