Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kukamatwa kwa dada wa aliyekuwa
Gavana wa Benki Kuu, Tanzania marehemu Daudi Balali, Elizabeth Balali
kwa kuruka dhamana na kukwamisha kuendelea kwa kesi inayomkabili kwa
zaidi ya miezi mitano.
Mshtakiwa huyo pamoja na mdhamini wake wameshindwa kufika mahakamani kwa kipindi chote hicho bila kuitaarifu mahakama.
Uamuzi
huo umetolewa leo Aprili 27, 2020 na Hakimu Mkazi Mfawidhi Godfrey
Isaya wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya mshtakiwa Elizabeth kusoma
maelezo ya awali lakini imeshindikana kwa kuwa mshtakiwa huyo hakuwepo
mahakamani.
Mapema Wakili wa Serikali Faraji Nguka alidai
mahakamani hapo kuwa, shauri hili leo lilikuka kwa ajili ya kumsomea
mshtakiwa maelezo ya awali lakini wote yeye na mdhamini wake hawakufika
hivyo aliiomba mahakama itoe hati ya kumkamata.
Hata hivyo, Hakimu Isaya alisema hati ya kukamatwa kwa mshtakiwa huyo ilishatolewa.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 26, 2021.
Awali
Elizabeth alikuwa akikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi
yaliyomfanya akae gerezani zaidi ya miezi sita kabla hayajafutwa na
kusomewa mashtaka mapya ya kujipatia Sh milioni 25 kwa ulaghai.
Kwa
mujibu wa hati ya mashtaka ya sasa Mshtakiwa huyo anadaiwa kati ya
Oktoba 19 na Desemba 21, 2017 katika Mkoa wa Dar es Salaam alijipatia
kiasi cha Sh milioni 25 kutoka kwa Dk Roderick Kisenge kwa njia ya
ulaghai baada ya kujifanya anamuuzia eneo la mita za mraba 900 ambalo
halijapimwa katika eneo la Boko Dovya Kinondoni wakati akijua eneo hilo
si lake.
Mshtakiwa alikana mashtaka na mahakama ilikubali kumpa
dhamana ambapo alidhaminiwa na mdhamini mmoja aliyesaini dhamana ya
maandishi ya Sh milioni tisa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...