Na,Jusline Marco:Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndg.Jerry Muro ametoa siku 30 za mazungumzo ya familia ya Losujake Sung'are ikiwa ni pamoja na kuifunga njia ambayo ilikuwa ikitumiwa na mmoja wa wanafamilia hao.
Hatua hiyo imefuatia kutokana na kuwepo kwa mgogoro wa ardhi baina ya wanafamilia hao ambapo Mkuu huyo wa Wilaya ameagiza kufungwa kwa njia hiyo baada ya kujiridhisha pasipo shaka kuwa ipo njia nyingine ya umma ambayo itamuwezesha kupita na mahakama itakapotoa hukumu.
"Eneo hili halitapita tena mtu mpaka hapo mahakama itakapoamua,wewe mama hutapita yena hapa na wewe kijana hutakanyaga kwenye hii nyumba mpaka mahakama itakapotoa maamuzi."Alisisitiza Mkuu huyo wa wilaya
Aidha Muro alieleza kuwa ametoa uamuzi huo baada ya kuzunguka eneo na kujiridhisha pasipo shaka kuwa ipo njia nyingine ya umma ambayo anaweza kupita ambapo amesema mamlaka hiyo anayo kwani sheria ya usalama wa yaifabinampa nguvu kuzuia ili watu wasiendeleze mgogoro kwa kipindi hicho alichokitoa.
Awali Mkuu huyo akisikiliza malalamiko ya pande zote mbili aliwataka wanafamilia hao kutouza maeneo yao ya urithi baada ya mgogoro huo kuisha kwani kila mmoja anastahili kupata haki sawa na mwingine kutoka katika urithi wa wazazi wao na kusema kuwa mgogoro unatokea pale mtu mmoja anapotaka kupata sehemu mara mbili ambapo amemtaka kila mmoja kuridhika na alichonacho.
Kwa upande wa wanafamilia hao aliejitambulisha kwa jina la Withness Osujake mama mdogo wa Olais Osujake amesema kuwa hajaridhishwa na uamuzi alioutoa Mkuu huyo wa Wilaya wa kumzuia kupita akidai kuwa hana mahali pengine pa kupita ili hali Olais Osujake alitenga njia mbadala ya mama huyo kupita.
Alieleza kuwa kitu kilichokuwa na mgogoro siyo barabara bali ni nyumba hivyo ataendelea kupita katika barabara hiyo ambapo ameiomba serikali imsaidie ili aweze kupata haki yake.
Naye Olais Osujake Laizer ambaye eneo lake ndilo yenye mgogoro ameunga mkono maamuzi aliyoyatoa Mkuu wa Wilaya hiyo ya kumzuia kwa muda wa siku 30 mama huyo kupita katika njia iluyopo kwenye eneo lake na yeye kutoingia katika nyumba hiyo yenye mgogoro mpaka pale watakapo weka mambo yao sawa na mahakama kutoa maamuzi kwani mama huyo amekuwa akitoa kauli za matusi wakati anapopita katika eneo hilo ameiomba serikali kumsaidia ili aweze kupata haki yake.
Kwa upande wake Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha,Bi.Eliasifiwe Kileo amesema kuwa suala lolote linapofikishwa mahakamani kinachotakiwa kutekelezwa ni maamuzi ya mahakama hivyo amewataka wanafamilia hao kufuata amri iliyitolewa na mahakama ya kurudia kusikiliza utekelezaji wa amri ya baraza la kata katika baraza la ardhi la nyumba la wilaya.
Pamoja na hayo Kaimu Mkuu wa Idara ya Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Arusha,Bi.Hadija Ntimizi amesema kuwa migogoro mingi ya ardhi inatokana na maeneo kutorasimishwa hivyo kutokana na mgogoro huo amesema kuwa eneo hilo halina njia katikati.
"Moja ya kanuni katika urasimishaji kila kipande cha ardhi kifikike ili kuweza kutoa urahisi wa huduma pindi majanga yanapotoa ikiwa ni pamoja na kutokomeza vichochoro."Alieleza Bi.Hadija
Katika hatua nyingine Muro amesitisha ujenzi wa nyumba na utaratibu wa kuomba maeneo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba katika maeneo katika eneo lililowazi kwa muda wa siku 7 hadi atakapokaa na kuzungumza na uongozi wa halmashauri,wakala wa mbegu ASA pamoja na wakaazi walio katika maeneo hayo.
Muro ameleza kuwa lengo ni kutafuta ukweli kama wakala wa mbegu ASA wametoa eneo hilo kwa Halmashauri na baada ya upimaji wa eneo hilo halmashauri waliweza kutoa kipaumbele kwa wananchi wanaokaa katika eneo hilo au lah!ikiwa ni pamoja na kutaka kufahamu kama Halmashauri imepima na kuuza viwanja.
"Katika hatua ya awali tumesitisha chchote hapa mpaka serikali ya wilaya itakapomaliza kulichunguza jambo hili na kuja kutoa taarifa rasmi kwenu wananchi ya nani anamiliki nini na nani ni nani katika eneo husika."Alieleza Muro.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha,Ndg.Jerry Muro katikati akitoa ushauri kwa familia ya mzee Osujake ili kuweza kupata utatuzi katika mgogoro wa ardhi kwenye familia hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Jerry Muro akiwataka wakazi wa Ngaramtoni walio katika eneo lililokuwa likimilikiwa na wakala wa mbegu ASA kuwa na subiri wakati serikali ya wilaya ikifanya mazungumzo na ASA pamoja na Halmashauri ya Arusha kuweza kubaini eneo hilo kama limepimwa na ninani miliki halali wa eneo hilo ili kuweza kutoa fursa kwa wakazi hao kununua eneo hilo na kujenga makazi yao.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akiwa na wanafamilia wenye mgogoro wa nyumba,mali ya marehemu mama yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...