Na Jusline Marco,Arusha

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Kenan Kihongosi amevitaka vikundi 42 vilivyomo ndani ya jiji la Arusha kuwa wazalendo kwa kuhakikisha wanarejesha kwa wakati mkopo wa shilingi milioni 565.3 walizopatiwa na Halmashauri ya jiji la Arusha kwa uaminifu.

Akifungua mafunzo ya vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kwa niaba ya Mkuu huyo wa Wilaya,Afisa Tarafa,tarafa ya Ererai Titho Cholobi amevitaka vikundi hivyo kutumia vyema mafunzo hayo ili yaweze kuwasaidia katika utumiaji wa mikopo hiyo.

Cholobi alisema kuwa fedha hizo zinatokana na mapato ya ndani ya halmashauri na kusema kuwa mikopo hiyo haitolewi kwa watu kujuana bali hutolewa kwa vikundi kufuata utaratibu uliopo ambapo amewataka vijana kujifunza kuaminika kwani fedha zinazotolewa ni fedha za walipa kodi ambazo zinapaswa kurejeshwa kwa wakati ili ziweze kukopeshwa watu wengine.

Adhia alisema kuwa halmashauri imekusudia kuweka mpango mkakati wa ufuatiliaji wa fedha shilingi bilioni 3 ambazo zilikopeshwa kwa wanavikundi na hazikurejeshwa hivyo ameyataka makundi hayo kufanya kwa uaminifu ili waweze kurejesha fedha hizo.

"Hii milioni 565.3 mnauopewa kama mkopo baadhi ya halmashauri ndiyo mapato yao ya ndani hivyo mkatumie fedha hizo katika kusudi lililokusudia ili muweze kurejesha kwa uaminifu zaidi."alisema Cholobi

Akitoa taatifa ya mikopo katika jiji la Arusha,Mkuu wa Idara ya maendeleo ya jamii jiji,Mwanamsiu Dosi amesema halmashauri imeendelea kutenga fedha kutoka katika mapato ya ndani ya halmashauri na kuelekezwa kwenye vikundi vya vijana,wanawake,na makundi maalum.

Aliongeza kuwa fedha zinazotolewa ni fedha za miezi 6 za robo ya kwanza na robo ya pili ambapo zitabaku fedha za robo ya 3 na robo ya 4 katika utoaji wa mikopo na kusema kuwa mikopo hiyo inayotolewa inapaswa kurejeshwa na haitokani na fedha za ruzuku.

Mmoja wa wanavikundi hao aliyejitambulisha kwa jina la Neema Noel ameishukuru halmashauri hiyo kwa kuweza kuwapatia mkopo huo ambao amesema utamsaidia kuendeleza biashara yake.

Kwa upande wake Afisa vijana jiji la Arusha kwa niaba ya Afisa maendeleo ya jamii wa jiji hilo,Hanifa Ramadhani amesema kuwa kwa kipkndi cha mwezi Juni hadi Desemba halmashauri imeidhinisha utoaji wa mikopo yenye zaidi ya shilingi milioni 565  kwa vikundi 42 Bya wajasiriamali vilivyopo katika kata 23 za jiji la Arusha.

Aliongeza kuwa kati ya fedha hizo zaidi ya milioni 359 zitatolewa kwa vikundi 25 vya wanawake na zaidi ya shilingi milioni 175 zitatolewa kwa vikundi 15 vya huku fedha zaidi ya milioni 30 zitatolewa kwa vikundi 2 vya watu wenye walemavu amnapo amwsema vikundi hivyo ni vile vilivyopitishwa na kamati ya fedha na utawala.

Pamoja na hayo amesema kuwa halmashauri itaendelea kutoa mikopo kwa kadri itakavyokuwa ikipokea maombi kutoka kwenye vikundi na kulingana na fedha zitakazokuwa zikipatikana kutokana na makusanyo ya mapato ya ndani ya halmashauri na marejesho ya mikopo ya nyuma .

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Jiji la Arusha,Mwanamsiu Dosi akitoa maelezo ya fedha ambazo zimeyolewa na halmashauri ya jiji la Arusha kwa wajasiriamali,kushoto ni Afisa tarafa wa tarafa ya Ererai Titho Cholobi na kulia ni Afisa vijana jiji la Arusha Hanifa Ramadhani,wakati wa utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu robo ya kwanza na ya pili ya mwaka wa fedha 2020/2021.
Afisa Tarafa,tarafa ya Ererai Titho Cholobi akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo kwa wajasiriamali wa vikundi 42   vilivyomo ndani ya jiji la Arusha.
 Wajasiriamali jiji Arusha wakipatiwa elimu ya matumizi ya fedha ambazo wanatarajia kuzopokea zaidi ya milioni 565.3 kutoka halmashauri ya jiji la Arusha kama mkopo kwenye kwa vikundi vilivyokidhi vigezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...