Shaka Hamdu Shaka ameteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi  Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushika nafasi ya Mtangulizi wake Hamfrey Polepole. Ameteuliwa leo jijini Dodoma mara baada ya Mkutano Mkuu wa Chama hicho Kumchagua Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan.

KATIBU Mkuu wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM)- Ndg Daniel Chongolo (Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Kinondoni) na Naibu Katibu Mkuu  Chama Cha Mapinduzi(CCM)ni Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Christina Mdeme.

Katibu wa Itikadi na Uenezi  Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka, ameshika nafasi ya aliyekuwa Katibu mkuu wa chama hicho, Hamfrey Polepole.

Katibu wa Uchumi na Fedha  Chama Cha Mapinduzi (CCM), Frank George Hawasi aendelee na nafasi yake, Katibu wa Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ngebela Lubinga anaendelea na nafasi yake.

Katibu wa Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) Oganaizesheni, Mama Maurdin Kastiko, ameshika nafasi ya Pereira Silima ambaye atapangiwa kazi nyingine ya kitaifa).

(Ndg Rodrick Mpogolo atapangiwa majukumu mengine ya kitaifa)

Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Juma Sadala Mabodi nae anaendelea na nafasi yake ya awali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...