Afisa Mtendaji wa Kata ya Dung'unyi wilayani, Ikungi mkoani Singida, Yahaya Njiku (kushoto) akikabidhi madawati kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Munkinya, katika hafla iliyofanyika juzi.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Dung'unyi, Yahaya Njiku, akizungumza na Walimu pamoja na Wanafunzi katika hafla hiyo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Munkinya, Faraja Mlelwa, aliwashukuru wadau wa maendeleo waliochangia upatikanaji wa madawati hayo.
Afisa Elimu wa Kata ya Dung'unyi, Ester Mkoma, akizungumza katika hafla hiyo.
Wanafunzi wakiwa katika hafla ya kupokea madawati hayo.









Na Dotto Mwaibale, Singida



KATA ya Dung'unyi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida imetekeleza agizo la Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutengeneza madawati na kuhakikisha wanafunzi wote walioanza kidato cha kwanza mwaka huu wanakwenda shuleni na wanakaa kwenye viti.

Madawati hayo yamepatikana kutokana na nguvu za wananchi.

Akizungumza jana wakati akikabidhi madawati hayo Afisa Mtendaji wa Kata hiyo, Yahaya Njiku aliwapongeza wananchi kwa kutengeneza madawati hayo kwa nguvu zao.

Alisema hatua hiyo waliifikia kufuatia ongezeko kubwa la ufaulu wa watoto na kuhakikisha wote wanakwenda shuleni na kuwa na viti vya kukalia.

" Leo nakabidhi madawati mapya 18 hapa Shule ya Sekondari Munkinya katika kata hii ya Dung'unyi ikiwa ni awamu ya pili baada ya awamu ya kwanza kukabidhi madawati 20 na idadi ya madawati yote kufikia 38 huku madawati zaidi ya 70 yakikarabatiwa." alisema Njiku.

“Kwa nchi nzima halmashauri yetu imekuwa ya 78 kati halmashauri 195 zilizopo kwa kutengeneza madawati tunakila sababu ya kujivunia na naamini kabisa ipo siku na sisi tutashika nafasi ya kwanza” alisema.

Mkuu wa shule hiyo ya Sekondari ya Munkinya, Faraja Mlelwa aliwashukuru wadau wa maendeleo waliochangia upatikanaji wa madawati hayo na kuwa watayatunza.

Lengo la halmashauri hiyo ni kuhakikisha madawati yote 3900 yanayohitajika yanapatikana na kuwa watoto wote wanafika chuo kikuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...