Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
KATI
ya watoto 100 wenye umri chini ya miaka mitano mkoani Pwani,watoto 24
wana Udumavu na hii imetokana hasa na familia zao kuwa duni hivyo
kushindwa kuinua uchumi wa familia hizo.
Pamoja
na hilo, hali ya usajili katika mfuko wa Bima ya afya ya jamii
(CHF)hairidhishi ,hadi sasa ni kaya 10,038 pekee sawa na asilimia 5.1
zimejiunga na mfuko huo kati ya kaya 294,634 .
Mkuu
wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,aliyaeleza hayo katika
kikao cha tathmini ya tatu ya utekelezaji wa mkataba wa lishe mkoani
hapo.
Alieleza ,hali ya udumavu kwa mkoa ni 23.8 ukilinganisha na ule wa Taifa 30.1.
Hata
hivyo alifafanua kwamba ,tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe
kwa kipindi cha Julai hadi Disemba 2020 ulivyotekelezwa ngazi ya
halmashauri ni halmashauri sita ndizo zilizofanya vizuri.
"Utoaji
wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za lishe ni sh.1,000 kwa
kila mtoto kwa mwaka na halmashauri sita zimetoa zaidi ya asilimia 90.
Ndikilo
alielezea, halmashauri tatu ikiwemo Mafia hali hairidhishi na ina
asilimia 28.8 tu,Kibaha Mji 79.1 na Kibiti asimilia 58.5.
Hata
hivyo ,mkuu huyo wa mkoa,alieleza hali duni husababisha kinga ya mwili
kuwa duni na kudumaa ,hivyo mwili hushindwa kupambana na vimelea vya
magonjwa mbalimbali ,Ili kupunguza gharama kubwa za matibabu ni muhimu
kila kaya kujiunga na mfuko wa Bima ya afya ya jamii (CHF).
Mkuu
wa wilaya ya Kibiti GulamHussein Kifu alisema ukiwepo,upungufu wa dawa
kwenye vituo vya huduma ya afya inachangia kuwepo na muitikio mdogo kwa
wanaojiunga na ICHF.
Nae
Mganga mkuu wa mkoa wa Pwani ,dkt.Gunini Kamba alibainisha, uhaba wa
dawa sio wa kutisha hivyo unafanyika utaratibu wa kuhakikisha dawa
zinapatikana kwa wingi kwenye zahanati na maduka ya dawa yaliyopo kwenye
hospitali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...