Na Mwamvua Mwinyi,Pwani


MKUU wa Mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo ametoa agizo na angalizo kwa madaktari na watumishi wa afya katika vituo vya afya na zahanati hususan vijijini ,kuacha tabia ya kufunga vituo mapema na atakaebainika kufanya hivyo atakuwa amejifukuza kazi .

Aidha amewaelekeza waganga wakuu wa wilaya kujenga utaratibu wa kutembelea vituo vya afya na zahanati zote ili kujua hali ya huduma zinazotolea.

Mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo ,alitoa maagizo hayo katika kikao cha wadau wa afya mkoani humo ,kilichofanyika Kibaha .

Alieleza,yapo malalamiko mengi ya uhaba wa dawa ,vifaa tiba na kufungwa kwa baadhi ya vituo vya afya ama zahanati."Haikubaliki ,hii inaweza ikawa sababu ya jamii kushindwa kujiunga na mfuko wa Bima ya afya ya jamii CHF ," alifafanua Ndikilo

Kwa upande wake ,mwenyekiti wa halmashauri ya Bagamoyo ,na Diwani wa kata ya Yombo Muhammed alieleza kuwa ,tatizo la dawa na kufungwa kwa vituo linasababisha kuzorota kwa huduma za afya.

Usinga alibainisha, kuna haja ya waganga wakuu kufuatilia watumishi wa ngazi ya chini na kujua hali ya huduma ikiwemo upatikanaji wa dawa na vifaa tiba na idadi ya watumishi badala ya kusubiri kupelekewa taarifa.

Nae mganga mkuu wa mkoa wa Pwani, dkt .Gunini Kamba aliwataka watumishi wa afya ,wote kuzingatia maadili ya kazi yao na kujituma kazini bila kufunga vituo vya afya suala ambalo ni kero.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...