Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
KERO ya huduma za Maji zilizokuwa zinaikumba Shule ya Sekondari Magole iliyopo jijini Dar es Salaam zimetatuliwa baada ya Shule hiyo kuchimbiwa Kisima kilichogharimu kiasi cha pesa taslimu Milioni Nane na Nusu (Tsh 8,500,000/-) zilizofadhiliwa na Taasisi ya Direct Aid Society.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa Maji, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omar Kumbilamoto amewataka Wanafunzi wa Shule hiyo kuulinda Mradi huo wa Maji pamoja na kusoma kwa bidii ili kufikia malengo yao katika maisha ya baadae.
Kumbilamoto amesema wataendelea kutatua changamoto nyingine kama upatikanaji wa Walimu wa masomo ya Sayansi, huku akiwahimiza kusoma kwa bidii na malengo ili kufikia lengo la kujaza nafasi za Walimu hao.
“Licha ya kupata Kisima, tunajua bado kuna Zahanati haijajengwa, kwenye Akaunti ya ujenzi wa Zahanati kuna zaidi ya Milioni 180 lazima kujengwe Zahanati katika Kata hii ya Mzinga ili kuhakikisha changamoto zote za matibabu zinatatuliwa kwa Wananchi wote”, amesema Kumbilamoto.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Taasisi ya Direct Aid Society, Miraji Mussa amesema wametekeleza mradi huo baada ya kuona changamoto kubwa ya upatikanaji Maji katika Shule hiyo, amesema Wanafunzi wanapaswa kuweka sawa na safi mazingira ya Shule yao ili kuvutia zaidi licha ya kuchimbiwa Kisima cha Maji.
Diwani wa Kata ya Mzinga, Job Isaac amewaasa Wanafunzi kusoma kwa bidii, na kumuomba Mstahiki Meya, Kumbilamoto kuhakikisha upatikanaji wa Maabara, Madarasa na Walimu katika Shule hiyo ya Magole.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam, Omar Kumbilamoto akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Magole kabla ya kuzindua Mradi wa Maji Shuleni hapo.Katibu Mkuu wa Taasisi ya Direct Aid Society, Miraji Mussa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Maji katika Shule ya Sekondari Magole jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...