Mkurugenzi wa TEWW Dkt. Michael Ng’umbi akizungumza katika mkutano wa kujadili na kutoa maoni kuhusu Mkakati wa Elimu Msingi na Mafunzo ya Watu Wazima (ABET) Ili kuboresha utekelezaji na uendeshaji wa programu za elimu ya watu wazima
Mweshaji
kutoka TEWW Bi. Leonia Kassamia akizungumza wakati wa mkutano kujadili
na kutoa maoni kuhusu Mkakati wa Elimu Msingi na Mafunzo ya Watu Wazima
(ABET) Ili kuboresha utekelezaji na uendeshaji wa programu za elimu ya
watu wazima.
Washiriki
wa mkutano wa kujadili na kutoa maoni kuhusu Mkakati wa Elimu Msingi na
Mafunzo ya Watu Wazima (ABET) Ili kuboresha utekelezaji na uendeshaji
wa programu za elimu ya watu wazima. Mkutano huo uliofanyika Mjini
Morogoro Aprili 28 na 29, 2021.
******************************
Na Mwandishi wetu- TEWW
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa kushirikina na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na TAMISEMI imeandaa Mkakati wa Elimu Msingi na Mafunzo ya Watu Wazima (ABET) Ili kuboresha utekelezaji na uendeshaji wa programu za elimu ya watu wazima.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Dkt. Michael Ng’umbi katika kikao kazi cha wadau kujadili na kutoa maoni kuhusu Mkakati huo kilichofanyika mjini Morogoro Aprili 28 na 29, 2021.
“Mkakati huu unatoa muongozi kwa wadau wa elimu nje ya mfumo rasmi kuhusu uendeshaji wa programu za elimu ya watu wazima, Commitment level, Financial support, Assessment system, Administrative structure na Innovation kwanzia ngazi ya wizara hadi serikali za mitaa,”alieleza Dkt. Ng’umbi
Akifafanua amesema, mkakati huo una himiza kutambua kwa wahitumi wa elimu nje ya mfumo rasmai kwa uwezo wao na kupewa fursa ya kushiriki katika shughuli za maendeleo ya taifa.
Wadau wa elimu nje ya mfumo rasmi walioshiriki katika kikao hicho ni wataalam wa elimu nje ya mfumo rasmi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, TAMISEMI, UNESCO na maafisa Elimu ya watu wazima kutoka mikoa ya Mwanza, Tabora, Dodoma, Arusha, Singida na Mbeya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...