NA YEREMIAS  NGERANGERA…NAMTUMBO.

Madiwani wa  Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo  mkoani Ruvuma  wamelalamikia kitendo cha wakulima wa korosho  wilayani Namtumbo kupeleka korosho zao  wilaya ya Tunduru  katika chama kikuu  cha TAMCU  kila mwaka badala ya kuuzia Namtumbo katika  chama kikuu  cha SONAMCU.

Wakiongea  katika kikao cha kamati  ya fedha uongozi na mipango cha Halmashauri hiyo diwani wa kata ya Magazini  Grace   kapinga  alidai kitendo  cha wakulima wetu , sisi wenyewe kuendelea  kuuza  mazao katika chama kikuu cha wilaya ya Tunduru TAMCU  sio sahihi.

Grace  alisema  kiwango  kinachozalishwa  korosho  katika wilaya ya Namtumbo ni kikubwa sana  hakuna sababu ya  kuendelea kupeleka korosho hizo katika  wilaya ya Tunduru  kwa  kuwa kuna chama kikuu SONAMCU wanaweza  kununua korosho hizo  katika wilaya yetu  kama wanavyofanya mazao ya stakabadhi ghalani alisema kapinga.

Afisa  kilimo na ushirika wa Halmashauri  ya wilaya ya Namtumbo  bwana  Joseph  Mbilinyi  alidai uwezekano  wa kuuzia  katika chama kikuu cha SONAMCU  utakuwepo  endapo  uzalishaji  wa zao la korosho katika wilaya ya Namtumbo  utavuka  tani 1000 na kuwepo  kwa maghala ya kuhifadhia  korosho  wakati wa mauzo .

Bwana Mbilinyi  pamoja na mambo mengine alisema  hana tatizo na kuwepo kwa  maghala ya kuuzia zao la korosho  katika wilaya ya Namtumbo  bali tatizo ni kukidhi  kigezo cha kuwa na uzalishaji  unaoanzia  tani 1000 na kuendelea  kadiri  ya mwongozo .

Afisa  ushirika  wa Halmashauri ya  wilaya ya Namtumbo  bwana  Emmanuel  Gwao  alitoa takwimu za uzalishaji  wa zao la korosho za kutoka wilaya ya Namtumbo  zilizouzwa  wilaya ya Tunduru  kwa msimu wa 2020/2021 kuwa ni tani 321 na kg 931 na   tani 500 kwa musimu wa 2019/2020.

Hata hivyo aliongeza  kuwa  wapo wananchi  katika vijiji  vya wilaya ya Namtumbo wanaozalisha korosho  kwa kiwango kidogo hawapeleki  katika masoko  kutokana na umbali wa kuuzia zao lenyewe  hivyo kama kutakuwa  na utaratibu wa kupata  soko  la kuuzia korosho  wilayani Namtumbo tutawashawishi  wananchi wengine wasio  katika mfumo rasmi  wa kuuza  zao la korosho kujiunga katika mfumo rasmi  ili kuongeza  uzalishaji  wa  zao hilo na kukidhi vigezo vya kufika kilo 1000 zinazohitajika .

Naye diwani  wa kata ya Limamu Isdory  Nyati  alisisitiza swala la ukusanyaji wa  mapato  hasa kwa kuhakikisha mabasi yanayotumika  kubeba mazao  kudhibitiwa  huku akiyataja  mabasi hayo kuwa ni Kangaulaya  na Kisumapai  yanayofanya  biashara ya kubeba abiria na mizigo kutoka    mamlaka  ya mji mdogo wa Lusewa   kwenda  Songea  na kuipotezea  ushuru  Halmashauriya wilaya ya Namtumbo.

Katibu  tawala wa wilaya ya Namtumbo bwana  Aden  Nchimbi  pamoja na kuwapongeza  madiwani  hao kwa kufuatilia kwa makini magari ya abiria yanayotumika  kubeba  mizigo  badala ya kubeba abiria  kuwa atahakikisha  anasimamia  swala hilo kwa makini ili kudhibiti  magari hayo yasiendelee kufanya hivyo  .

Halmashauri  ya wilaya ya Namtumbo ina tegemea  ushuru wa mazao  katika ukusanyaji wake  wa mapato  na kuwepo kwa  mianya ya utoroshaji  wa mazao  kwa njia ya mabasi  inaipotezea  ushuru  Halmashauri  wilaya ya Namtumbo  na kupeleka  songea.


 Diwani wa kata ya magazini Grace Kapinga akiwasilisha malalamiko ya kuuzia zao la korosho wilaya ya Tunduru na kutaka zao hilo liuziwe chama kikuu cha SONAMCU na sio TAMCU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...