Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Said Jafo amesema atahakikisha changamoto za Muungano zilizosalia zinapatiwa ufumbuzi.

Ameyasema hayo hii leo mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Makamu wa Rais na kukutana na Menejimenti ya Ofisi yake na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini.

"Nashukuru kwa mapokezi mazuri, ila tuchape kazi tunahitaji kupata matokeo chanya kwa kazi tunazo simamia yaani Muungano na Mazingira" Jafo alisisitiza.

Kwa upande mwingine Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Hamad Chande amesisitiza ushirikiano baina ya watumishi katika kuhakikisha malengo ya kudumisha Muungano na kusimamia Mazingira yanatekelezeka.

Akiwasilisha taarifa ya Ofisi yake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo amewahakikishia ushirikiano Mawaziri na kuwakarisha kwa niaba ya watumishi wenzake.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...