Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa maelezo kuwa  serikali imepokea na itayafanyia kazi  malalamiko ya wabunge juu ya utaratibu  wa ukaguzi  kwenye mgodi wa  Mererani, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 29, 2021. (Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu)

********************************

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imepokea na itayafanyia kazi  malalamiko ya wabunge juu ya utaratibu  wa ukaguzi unaofanywa kwenye mgodi wa  Mererani,

“Nimesikia concern ya namna ukaguzi unavyoendelea pale katika mgodi wa Mirerani, nilipanga kutembelea Mirerani ili kuona hali hiyo na kutafuta ufumbuzi, nikuahidi Mhe. Spika na waheshimiwa wabunge kwamba tumepokea na Serikali tutalifanyia kazi,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Aprili 29, 2021) wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka ambaye ambaye alitaka maelezo juu ya utaratibu wa ukaguzi katika mgodi huo. Mbunge huyo alikuwa akichangia mjadala wa hotuba makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Madini.

Amesema Serikali inapata fedha nyingi kupitia madini ya Tanzanite yanayochimbwa katika mgodi huo hivyo haiwezi kushindwa kununua mtambo unaoweza kufanya ukaguzi wenyewe bila kusumbua mtu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...