Na Mwandishi wetu, Kiteto
MBUNGE
wa viti maalum wa Mkoa wa Manyara, Regina Ndege amegawa taulo za kike
505 kwa wasichana wanafunzi wa shule ya Sekondari Engusero Wilayani
Kiteto na mipira miwili kwa ajili ya kucheza mpira wa miguu kwa wavulana
wa shule hiyo.
Ndege
ambaye kitaaluma ni mwalimu ameyasema hayo kwenye ziara yake ya
kutembelea Wilaya ya Kiteto ambapo pia alizungumza na Baraza la wanawake
wa Jumuiya ya UWT.
Amewaasa wasichana hao wasome kwa bidii kwani changamoto ya taulo za kike watakuwa wameondokana nayo kwa sasa.
Hata
hivyo, amewataka wavulana wa shule hiyo kusoma kwa bidii na kushiriki
michezo wakati wa mapumziko ndiyo sababu akawapa mipira hiyo miwili ya
mpira wa miguu."Naahidi
kuwa mstari wa mbele kuwasemea zaidi na kuwa mtetezi wa wanafunzi
Bungeni katika changamoto mbalimbali zinazowakabili hasa kwenye suala
zima la elimu," amesema Ndege.
Hata
hivyo, wanafunzi hao wamemshukuru kwa kuwezesha kuwapa taulo hizo za
kike ambazo kwa namna moja au nyingine zitapungusa changamoto ya sodo.
"Taulo
hizi zitatusaidia wanafunzi kuendelea na shule kuepuka na kukaa
nyumbani na kukosa masomo siku muhimu katika ukuaji huo," amesema mmoja
kati ya mwanafunzi aliyepatiwa taulo.
Kwa
upande wao wanafunzi wanafunzi wavulana walishukuru kwa kupatiwa mipira
hiyo miwili ambayo watakuwa wanaichezea pindi wakiwa kwenye mapumziko
baada ya masomo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...