Rais wa Mpira Kikapu TBF Phares Magesa akiwa na viongozi kampuni ya Premier betting jijini Dar es Salaam.
 

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

MAKUBALIANO hayo yalifikiwa katika kikao kilichowasisha Ndg. Sami Matar Mkurugenzi wa kampuni ya Premier Betting , James Mbalwe Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (Gaming Board of Tanzania - GBT) na Phares Magesa, Rais wa Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF.) 

Viwanja hivyo vitajengwa na kampuni ya Premier Betting kupitia mradi wa Premier Projects ikiwa ni sehemu ya kuridosha fadhila kwa jamii (CSR.) 

Kwa kuanzia kampuni hiyo ya Premier Betting itajenga uwanja wa kikapu Dar es Salaam itafuatia mikoa mengine yote nchini itafikiwa kwa awamu, utekelezaji wa mradi huu inatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa. 

Rais wa TBF ameishukuru kampuni ya Premier Betting kwa kukubali ombi la TBF kusaidia ujenzi wa viwanja nchini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji  wa moja ya melengo muhimu ya mpango kazi wa TBF katika kuinua mchezo wa kikapu nchini.

Magesa amemshukuru Mkurugenzi Mkuu wa GBT kwa kusimamia na kuhakikisha Premier Betting inafikia makubaliano na TBF na amewataka kutekeleza mradi huu haraka.

Ndg. Magesa alisema tayari wameshawasiliana na Mamlaka husika za Jiji la Dar es Salaam ili kupatiwa eneo ambako uwanja huo unatarajiwa kujengwa na pia ameziomba Halmashauri zote nchini kutenga maeneo ya viwanja vya michezo ili kila mkoa utakapofikiwa basi eneo la kujenga liwe tayari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...