MFUMO wa stakabadhi mazao ghalani katika Mkoa wa Ruvuma umewawezesha wakulima kupata fedha zaidi ya shilingi bilioni 28.

Akizungumza wakati anafungua mkutano wa wadau wa mazao ya ufuta,soya na mbaazi kwenye ukumbi wa Songea Club,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme  amesema kiasi hicho cha fedha kimepatikana  katika msimu wa masoko wa mwaka 2020/2021.

Ameyataja mazao yaliuzwa katika mfumo wa stakabadhi ghalani kupitia minada mbalimbali iliyofanyika katika wilaya za Songea,Tunduru na Namtumbo kuwa ni  ufuta,soya na mbaazi.

Kwa mujibu wa Mndeme,zao la ufuta kilo 12,234,737 zilizouzwa na kuwaingizia wakulima zaidi ya shilingi bilioni 25,soya kilo 1,499,077 ziliuzwa na kuwaingizia wakulima zaidi ya shilingi bilioni moja na zao la mbaazi kilo 4,260,77 ziliuzwa na kuwaingizia wakulima zaidi ya sh.bilioni 2.585.

“Mfumo wa stakabadhi mazao ghalani umeonesha mafanikio makubwa katika Mkoa wetu,hivyo leo tunafanya tathmini ya msimu wa masoko uliopita 2020/2021 na kuratibu maandalizi ya msimu wa masoko wa 2021/2022 ambapo ununuzi unatarajia kuanza Mei 2021’’,alisema Mndeme.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amesema  mfumo huo umeziwezesha Halmashauri kukusanya ushuru kwa lengo la kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo kupitia zao la ufuta pekee zilikusanywa zaidi ya sh.milioni 954 za ushuru kwenye Halmashauri.

Mafanikio mengine ya mfumo huo ameyataja kuwa ni kufufuliwa kwa vyama vingi vya ushirika,kuongeza ajira na kwamba mfumo umerahisisha ukusanyaji wa kodi kwa ajili ya mapato ya serikali kuu kupitia TRA.

Awali akitoa taarifa ya mazao ya ufuta,soya na mbaazi kwenye mkutano huo,Mrajisi Msaidizi wa Vyama Vya Ushirika Mkoani Ruvuma Bumi Masuba ameutaja uendeshaji wa masoko ya mazao hayo,ulifanyika kupitia vyama vya msingi 44 mkoani Ruvuma na kuleta mafanikio makubwa.

Ameyataja maandalizi ya masoko katika mkoa wa Ruvuma msimu wa 20201/2022 kuwa yanaendelea kufanyika kwa mfumo wa stakabadhi za ghalani kupitia vyama vya ushirika.

“Makadirio ya uzalishaji wa mazao hayo katika msimu huu ni ufuta tani 15,437,soya tani 7,844 na mbaazi tani 2,889’’,alisema Masuba.


 

 

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme  akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa mazao ya ufuta,soya na mbaazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Songea Club
wadau wa mazao ya soya,ufuta na mbaazi kutoka wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma wakiwa kwenye mkutano uliofanyika ukumbi wa Songea Club


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...