Na Amiri Kilagalila,Njombe

Serikali imewataka watanzania kudumisha amani mshikamano na umoja ili kuendeleza tunu za taifa na kujiletea maendeleo ya uchumi kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Wito huu umetolewa na waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Willium Lukuvu kwa niaba ya waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mazishi ya aliyekuwa Mhashamu Askofu Alfred Leonard Maluma wa jimbo katoliki la Njombe yaliyofanyika jimboni hapa.

Aidha ametoa wito kwa watanzani kuendelea kuliombea taifa pamoja na Rais Samia Suluhu ili kuendelea kuwa pamoja na kudumisha amani itakayoendelea kuleta umoja.

“Tunaomba madhehebu na watanzania wote,tuendelee kuiombea nchi yetu ili mwenyezi Mungu aendelee kutubariki tudumishe amani,upendo na mshikamano ili mwisho wa yote wananchi waweze kuishi kwenye nchi iliyo salama na yenye usawa”alisema Lukuvi

Ametoa wito kumuombea Rais “Tumuombee sana mheshimiwa Rais wetu wa awmu ya sita mama yetu Samia Suluhu Hassan amabye ameenza vizuri ili angalau aendelee kudumisha yale ambayo yameanzishwa na mtangulizi wake,atekeleza yale ambayo tunamatumaini nayo tunayajua yameandikwa kwenye Ilani yetu ya Chama cha Mpainduzi”alisema Lukuvi

Akitoa salamu za baba mtakatifu,Askofu wa jimbo katoliki la Songea mhashamu Damian Dallu ametoa wito kwa viongozi wa serikali kuendeleza jitihada na mapambano ya kiuchumi yalioachwa na hayati John Pombe Magufuli huku akimtangaza Askofu wa jimbo la Mbinga kuwa msimamizi wa kitume jimbo la Njombe mpaka hapo jimbo litakapopata askofu wake.

“Tarehe sita mwezi huu wanne Baba mtakatifu amemteua baba Askofu John Ndimbo wa Mbinga kuwa ndiye msimamizi wa kitume wa jimbo la Njombe”alisema Askofu Damian Dallu

Kwa upande wao viongozi wa dini mbali mbali akiwemo Askofu wa kanisala Kiinjili la Kilutheri Tanzania dayosisi ya kusini George Mark Fihavango na Shegh mkuu wa mkoa wa Njombe Rajab Msigwa wakitoa salamu zao kabla ya ibada ya mazishi wamemtaja hayati Askofu Malumu kuwa ni mtu aliyekuwa mpenda haki na maendeleo.


Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Willum Lukuvi mbele ya kanisa katoriki jimbo la Njombe akitoa salamu za serikali kwa niaba ya waziri mkuu na kuwashukuru wa Tanzania kuwa pamoja katika maombelezo ya aliyekuwa Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Wa kwanza kushoto ni waziri willium Lukuvi pamoja na viongozi mbali mbali akiwemo mmbunge wa jimbo la Ludewa wa kwanza kulia wakiwa katika ibada ya kuaga mwili wa hayati askofu Maluma wa Njombe.
Baadhi ya maaskofu wakiwa wamezunguka jeneza na kumuombea hayati Askofu Maluma kabla ya zoezi la mazishi.
Jeneza lenye mwili wa askofu Maluma lipelekwa katika eneo maalum la mazishi lililopo ndani ya kanisa katoliki jimbo la Njombe.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...