Na Woinde Shizza, Michuzi Tv -ARUSHA
SERIKALI wilayani Arumeru imefanikiwa kukamata mtandao wa watu wanaotajwa kuongoza mtandao wa kuvunja mabanda na mazizi ya wananchi na kisha kuiba Ng’ombe na mbuzi na kisha kuchinja usiku ambapo alfajiri hupeleka nyama mabuchani.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro kufanya operesheni ya pili ya siku tano za kuusaka mtandao huo, ambapo safari hii ilifanikiwa kuwakamata vijana wawili wakiwa pikipiki mbili wakitupa Ngozi pamoja na kitoto kichanga cha ng’ombe kilichofia tumboni baada ya kuchuna ngozi.

Wakizungumza katika eneo la tukio vijana hao wamesema wao hawana maelezo zaidi ya kuwa walitumwa na boss wao, ambapo katika tukio hilo baba mzazi wa kijana mmoja aliekamatwa amesema mazingira ya kukutwa na ngozi zikiwa mbichi na zilizochonwa katika mazingira ya wizi kunaongeza mashaka ya mwanae kuwa mmoja wa wahusika wa wizi.

Katika operation nyingine iliyofanyika katika tarafa ya Mukulati halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru, Dc Muro pamoja na vyombo vya usalama walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wengine nane wanaojihusisha na wizi huo ambao wamekiri kuhusika na wizi wa ng’ombe na mbuzi

Akizungumza na wananchi waliokusanyika katika kituo cha polisi cha usa river, mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro amewahakikisha wananchi hao serikali haitalala mpaka hapo changamoto ya wizi wa mifup itakapokwisha katika wilaya hiyo na kuendelea kusisitiza wazazi kuwafichua vijana wao wanaojihusisha na mitandao ya wizi.

Awali baadhi ya wananchi walioshiriki katika operesheni hiyo mbali na kupongeza kazi nzuri iliyofanywa na serikali ya wilaya ya Arumeru kulivalia njuga suala hilo, wamesema kuna haja ya kutazama upya sheria za uhalifu wa mifugo ili nazo ziboreshwe na kuwa kama sheria za matukio ya uhalifu wa kutumia silaha au mauaji.

Wilaya ya Arumeru imekuwa ikikumbwa na matukio ya mara kwa mara ya wizi ya mifupa na haswa katika matukio ya wananchi kuvamia majumba ya watu na kuvunja na kisha kuporwa Ng’ombe na mbuzi ambapo mpaka sasa kwa kipindi cha miaka miwili zaidi ya Ng’ombe 32 wameibwa katika maeneo mbalimbali wilayani Arumeru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...