Charles James, Michuzi TV

IKIWA leo ni Siku ya mwisho ya maombolezo ya siku 21 ya kifo cha aliyekua Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli wabunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wamewataka wanasiasa vijana kuepuka kuwa na ndimi mbili huku wakimtakia heri Rais Mama Samia.

Wakizungumza nje ya Bunge jijini Dodoma, wabunge hao Hawa Mwaifunga na Nusrat Hanje wamesema wanaamini  Rais Mama Samia ana uwezo wa kuiongoza nchi vizuri na kufanya vizuri kwani tayari alikuepo serikalini.

Akizungumzia suala la baadhi ya wanasiasa ambao wameanza kutoa kauli za tofauti na zile walizokua wakizitoa kipindi cha Dk Magufuli wakitolea mfano suala la Mbunge wa Nzega Vijijini, Dk Hamis Kigwangala kuhusu msimamo wake wa kujifukiza.

" Ni mshangao mkubwa kuona hata siku 21 za maombolezo hazijaisha watu waliokua wanamuunga mkono Dk Magufuli kuhusu kujikinga na ugonjwa wa Corona kwa kujifukiza.

Kwa sisi wanasiasa vijana tunapaswa tuchunge ndimi zetu kwa sababu watanzania waliotuchagua wametuamini sana kugeuka misimamo yetu ni kuwaonesha kwamba hatufai kupewa uongozi," Amesema Mwaifunga.

Amesema ana imani kubwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kuiongoza Tanzania na kwamba anaamini atafanya kazi kubwa ya kuwatumikia watanzania kwani anaifahamu Serikali.

Nae Nusrat Hanje amesema siku 21 za maombolezo zimeisha leo hivyo anaamini watanzania wamezitumia katika kuyaenzi mazuri yaliyofanywa na Dk Magufuli kwamba ana imani kubwa ya Rais Samia kufanya kazi nzuri ya kuiletea Nchi maendeleo.

" Hatuna shaka na Mama Samia katika kuwaendeleza yale yote ambayo aliyaanzisha Magufuli lakini anaweza kufanya makubwa zaidi kwani amekua sehemu ya Serikali kwa miaka sita," Amesema Nusrat Hanje.

Amewataka wanasiasa vijana waliobadilika misimamo yao ya Corona kujifunza kuwa na msimamo mmoja kwani kubadilika huko kunawavunjia heshima na kuwaondolea imani yao kwa Wananchi.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...