KATIKA Kuimarisha utendaji kazi na kuleta tija kwa jamii na Serikali
Naibu Waziri na Ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara amekutana na
Menejimenti za Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo Mkoani Dar es Salaam
na kujadili ubireshaji wa Wizara hiyo.
Katika kikao hicho, Waitara amepata nafasi ya kupokea taarifa mbalimbali za utekelezaji kutoka katika Taasisi hizo.
Aidha,
Waziri Waitara amezitaka taasisi hizo kufanya kazi kwa weledi na
ubunifu ili kuiwezesha Serikali kupata mapato ambayo yatasaidia katika
utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini.
Aidha ameahidi
kutembelea kila taasisi ili kujadiliana kwa kina juu ya utekelezwaji
wa majukumu, changamoto, mafanikio na mikakati ya kusonga mbele katika
kutekeleza majukumu ya wizara.
Vilevile Waitara amezitaka
menejimenti zote kuipitia upya hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipolihutubia Bunge na watanzania
wote Aprili 22, 2021 ili kuyachambua maono ya Mhe. Rais na kujipanga
vizuri kuyatekeleza.
Mkutano wa Naibu Waziri wa Ujenzi na
Uchukuzi Mhe. Mwita Waitara na menejimenti za Taasisi ni mkutano wa
kwanza tangu Mhe. Waitara alipoteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kushika nafasi hiyo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...