Makamo wa kwanza wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Othman Masoud Othman amesema Zanzibar inahitaji kuendelea na Umoja ili iwe rahisi kuleta maendeleo kwa wananchi wake

Kauli hiyo amaeitoa mara baada ya kukamilisha ziara ilioandaliwa na Chama cha ACT wazalendo kwa ajili ya kutembelea wagonjwa katik mkoa wa Kaskazini Unguja.

Makamu alisema hakuna njia nyengine itakayoweza kuleta maendeleo bila kuwepo mashirikiano, upendo na ummoja miongoni mwa Wazanzibar. Alieleza kuwa yupo tayari kutoa mchango wake kwa kuwatumikia wananchi kwani anamini nao wapo tayari kuendeleza upendo na amani juu ya nchi yao.

“Na mimi naweka ahadi ya kuwatumikia wazanzibar kwa wakati wowote ili kuendeleza yale yaliyoanzishwa na kuweza kuleta tija katika muendelezo wa kuyaimarisha zaidi” alisema Othamn.

Alisema anayoimani kwamba anaweza kutoa mchango wake katika kutumikia watu na kufanyakazi kwa moyo na wananchi wa ili malengo ya uwepo Umoja wa kitaifa uweze kufikiwa.

“Ili tupendane basi tuwe wamoja kwani umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu” alisema othaman. Alifahamisha kuwa umoja na upendo ndio silaha pekee ya uwepo wa amani kudumu katika taifa loloote lile duniani.

Alisema upendo na umoja huo unapendeza zaidi watu wakitembeleana na kusaidiena kwa wale wanaohitaji msaada.Kutokana na kauli hiyo aliwaomba wananchi wote kuwa na utamaduni wa kutembeleana kuazia familia, majirani pamoja na marafiki kwa lengo la kujenga upendo miongoni mwao.

Alisema mgonjwa yeyote akiona anatembelewa na jamaa zake au majirani, marafiki basi hujisikia faraja kupunguza maumivu ya maradhi.Sambamba na hilo aliwashauri wananchi wa Zanzibar hasa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kuftari kwa moja ili kuwa karibu zaidi na kuwastiri wale walikuwa hawana uwezo.

Alisema kuna watu wengi hawana Ftari lakini kama utamaduni kuftari kwa pamoja ndugu na majirani utaendelea basi utaleta faida kubwa miongoni mwao. Katika Ziara hiyo ya kuangalia na kuwafariji wagonjwa katika vijiji vya Mkoa wa Kaskazini Makamu wa Kwanza alitembelea wagonjwa katika Vijiji vya Chaani, Matemwe ,Nungwi, Kendwa, Kilimani Tazari, Mahonda ,Bumbwini Mafufuni, na Kiomba Mvua. 

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman akimuangalia na kumjulia hali na Kumfariji alyekuwa Mwakilishi wa Zamani wa chama cha wananchi CUF  Mzee Zahran Juma Mshamba kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya Kiharousi alipofika Nyumbani kwake Bumwini Mafufuni Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman akisalimiana na Viongozi wa ACT wazalendo Wiya ya Kaskazini B Unguja waliojitokeza kaika ziara iliyoandaliwa na chama cha  ACT wazalendo kwa ajili ya kuwatembelea wagonjwa na kuwafariji  Visiwani Zanzibar.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...